Sekta ya benki ya Rwanda imeshuhudia faida yake halisi kwa muda wa muongo mmoja. / Picha Benki ya Equity Rwanda

Sekta ya benki ya Rwanda kwa zaidi ya muongo uliopita umeonyesha utulivu wa jumla na ukuaji thabiti. Hii ni kulingana na ripoti.

Sekta ya benki ya Rwanda imeshuhudia faida yake halisi ikipanda kutoka Rwf71 bilioni ( dola miliomo 54) mwaka 2014 hadi zaidi ya Rwf bilioni 250 ( dola milioni 190) kufikia Septemba 2023.

"Benki zimeweza kudumisha mapato yao ya riba kupitia usimamizi mzuri wa hatari na mabadiliko ya kimkakati kuelekea mali isiyo na hatari," Tony Francis Ntore, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Mabenki cha Rwanda, RBA.

Wataalamu wanasema ukuaji huo mkubwa unachangiwa na viwango vya riba thabiti na ongezeko la mara kwa mara la mikopo iliyotolewa.

Kando na mtazamo wa tahadhari ambao benki zimekuwa nazo kuhusu ukopeshaji na usimamizi madhubuti wa hatari, Ntore pia alihusisha mwelekeo chanya wa benki na ufanisi wa uendeshaji na usaidizi mzuri wa udhibiti, ambao umesaidia utendaji wa jumla wa kiuchumi wa Rwanda.

Wadau wa sekta ya benki kwa kiasi fulani walihusisha faida kutokana na kuongezeka kwa malipo na mtiririko wa kutuma pesa nchini.

"Mbali na mikopo, ambayo ni biashara kuu ya benki, malipo na fedha zinazotumwa na fedha zimechangia faida ya sekta hii," alisema Carine Umutoni, Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Rwanda.

Takwimu zinaonyesha mtiririko wa kutuma pesa nyumbani kutoka nchi za nje, ulizidi uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni mwaka jana, na wataalamu wamesema unakwenda sambamba na kuonyesha jukumu ambalo benki hucheza katika kuwezesha mtiririko wa utumaji pesa.

TRT Afrika