Rwanda inalenga kuongeza mazaoa yake kutumia teknolojia ya kilimo / Picha: wizara ya Kilimo Rwanda 

Rwanda imeanza mradi wa miaka mitano wa kuboresha uzalishaji wa chakula kupitia kilimo nchini.

Mpango wa Kilimo wa Bayoteknolojia wa Rwanda unalenga kuongeza uzalishaji wa mihogo, mahindi na viazi.

Uwekezaji utagharimu dola milioni 10 (takriban Rwf13 bilioni) kuanzia Oktoba 2024 hadi Oktoba 2029.

Waziri wa Kilimo na Rasilimali za Mifugo, Ildephonse Musafiri, alisema Rwanda inakabiliwa na changamoto zinazozikumba nchi jirani, ikiwa ni pamoja na kukithiri kwa uvamizi wa viwavijeshi na ukame unaoathiri mahindi, ugonjwa wa michirizi ya kahawia kwenye mihogo, na mnyauko wa kuchelewa kakomaa viazi.

Uwekezaji huu wa bayoteknolojia utawawezesha wakulima wa Rwanda fursa ya kupata na kupanda mazao yenye mavuno mengi na kuwaepusha na hasara kutokana na wadudu na magonjwa yaliyopo.

Sheria ya Usalama wa viumbehai ya Februari 2024 nchini humo inalenga kuhakikisha kwamba viumbe vilivyobadilishwa vinasaba (GMOs) vinashughulikiwa, kuhamishwa na kutumika kwa usalama nchini Rwanda.

"Uwekezaji huu utawawezesha wakulima wa Rwanda kupata na kupanda mazao yenye mavuno mengi, na hivyo kuokoa mazao yanayopotea kutokana na wadudu na magonjwa," Waziri alisema.

Kulingana na taarifa kutoka wizara ya afya ya Rwanda serikali imefanya kazi pamoja na washirika wengine katika teknolojia ya mihogo, mahindi na viazi kwa miaka kadhaa ili kutatua changamoto za uzalishaji mdogo katika mazao haya.

TRT Afrika