Serikali ya Rwanda imeitisha sheria mpya kuhusu vikundi vya kijamii vya kuwekeza.
Maarufu kama 'tontine' kwa Kiingereza, huu ni mpangilio unaoruhusu wanachama kuweka akiba ya kiasi kidogo cha fedha au chama cha akiba na mikopo kinachozunguka.
Nchini Rwanda, vikundi hivyo vinaitwa "ibimina" na huundwa na watu wenye kitu kinachowaunganisha, kwa mfano, kina mama, watu wanaofanya kazi pamoja, watu wanaotaka kuchangia mradi mdogo wa pamoja na kadhalika.
Sheria hii mpya inayosimamia tontines - inayojulikana kama ibimina - inatarajiwa kuzuia usimamizi mbaya wa fedha zilizohifadhiwa na wanachama na kusaidia kuhakikisha uwajibikaji kwa ukuaji wa mifumo hii ya kifedha ya kijamii.
Agizo la mawaziri la Agosti 21, 2024, linalosimamia uundaji wa vikundi linatarajia, miongoni mwa mengine, kwamba vyama visajiliwe na usimamizi wa sekta ambayo inahudumu.
Serikali inasema kabla ya agizo hili, kulikuwa na masuala mengi, haswa kukosekana kwa mfumo wa kisheria. Sheria hii inasema kuwa wanachama sasa wanaweza kupata haki ya kisheria kupitia usajili, ambao unawapa haki ya kwa mfano, ya kushtaki mahakamani iwapo kuna tatizo.
Kanuni mpya inaruhusu wanachama wa vyama kuwa huru kuweka na kupitisha sheria zao za utaratibu. Hii, ni pamoja na mchakato wa usajilii.