Wadau katika sekta hii wanasema kuwa muda wa kupata vitambaa hivi unazidi miezi miwili, muda mrefu zaidi ya wiki mbili au nne inayofaa/ Picha Wengine 

Serikali ya Rwanda inatafuta wawekezaji ili kuendeleza uboreshaji wa ngozi katika eneo maalumu la kiuchumi la Bugesera.

Mpango huo, ambao unalenga kupunguza uagizaji wa ngozi zilizokatwa na pia kukuza sekta ya ngozi ya ndani, ulitangazwa mnamo 2021 na Wizara ya Biashara na Viwanda lakini haukuweza kutekelezwa kwa sababu ya uhaba wa fedha, pamoja na changamoto nyengine.

Uwekezaji unaopendekezwa kwa kiwanda jumuishi cha usindikaji wa ngozi, kilicho na vifaa vya kutibu maji taka, unakadiriwa kuwa na thamani ya dola milioni 15.1 (takriban Rwf 19.7 bilioni).

"Kiwanda cha kuboresha ngozi kinahitaji eneo ambalo liko mbali na shughuli za binadamu. Hii ni takriban umbali wa kilomita moja-ili kuzuia uchafuzi wa mazingira kuathiri maeneo jirani, kwani ni sekta inayochafua sana," Fred Mugabe, Mkurugenzi Mkuu anayeshughulikia Ukuzaji wa Viwanda na Maendeleo ya Ujasiriamali katika Wizara ya Biashara na Viwanda alielezea.

"Eneo tayari limetambuliwa, na hatua iliyofuata ilikuwa kutathmini faida ya biashara hii," Mugabe aliongeza, "Tumeanza kuwashirikisha wawekezaji."

Sekta ya nguo nchini Rwanda inakabiliwa na changamoto kubwa, hasa upatikanaji mdogo wa malighafi kama vile vitambaa na vifaa vya ziada. Wadau wengi katika sekta hiyo hutegemea vitambaa vinavyoagizwa kutoka nje, hasa vilivyofumwa kutoka China na vitambaa vilivyounganishwa kutoka kanda ya Afrika Mashariki, hasa Kenya na Uganda.

Wadau katika sekta hii wanasema kuwa muda wa kupata vitambaa hivi unazidi miezi miwili, muda mrefu zaidi ya wiki mbili au nne inayofaa.

Kulingana na takwimu rasmi za nchi hiyo bidhaa tano kuu za nguo zinazouzwa nje ya Rwanda (kwa thamani) ni pamoja na viatu vyenye mpira au soli za plastiki na nguo za juu, suruali za wanaume, jaketi au koti za wanawake zinazotengezwa na nyuzi zisizo za asili ( yaani synthentic), na pia za wanaume.

TRT Afrika