Rais Paul Kagame amekubali maafisa wa kijeshi wastaafu wakiwemo majenerali kumi na wawili.
Majina ya majenerali hao yaliorodheshwa katika taarifa iliyotolewa Jumatano.
Kati yao ni jenerali James Kabarebe ambaye amekuwa mshauri wa rais kwa maswala ya usalama.
Jenerali James Kabarebe pamoja na Luteni Jenerali Charles Kayonga wamewahi kuwa wakuu wa Majeshi wa taifa ya Rwanda.
Jenerali Kabarebe aliwahi kuwa waziri wa ulinzi kabla ya sasa kuwa mshauri mkuu wa rais katika masuala ya ulinzi na usalama.
Luteni Jenerali Frank Mushyo Kamanzi ni balozi wa sasa wa Rwanda nchini Urusi.
"Rais Kagame pia ameidhinisha kustaafu kwa maafisa wakuu 83, maafisa sita wa ngazi ya chini na maafisa wakuu 86 wasio na kazi. Pia wengine 678 ambao kandarasi zao zilimalizika na 160 kuachiliwa kwa matibabu,” taarifa ya kutoka kwa jeshi la Rwanda imesema.