Serikali ya Rwanda ilitangaza sheria inayosimamia misitu na miti, ambayo pamoja na vifungu vyengine, inakataza wakazi kuvuna ‘miti michanga.’
Serikali ya Rwanda inategemea kuingia katika soko la kimataifa la kaboni.
Masoko ya kaboni ni mifumo ya biashara ambayo mikopo ya kaboni inauzwa na kununuliwa.
Makampuni au watu binafsi wanaweza kutumia mipango kama hii kufidia uzalishaji wao wa gesi chafuzi kwa kununua mikopo ya kaboni kutoka kwa taasisi zinazoondoa au kupunguza utoaji wa gesi chafuzi.
Sheria mpya inachukua nafasi ya ile ya mwaka 2013 inayosimamia usimamizi na matumizi ya misitu. Inapanua wigo wa usimamizi wa miti na kuongeza mwelekeo wa upandaji miti, kilimo mseto, na upandaji miti kando ya mito, maziwa, barabara, na maeneo ya makazi ya mijini, miongoni mwa mengine.
Katika sheria ya mwaka 2013 leseni ya uvunaji wa misitu pekee ilitakiwa kwa msitu wenye ukubwa wa hekta mbili na zaidi lakini sheria hii ya mwaka 2024 inapinga leseni ya uvunaji wa misitu au miti katika maeneo yote - hata kama ni chini ya hekta mbili.
Sheria hii pia inasema ni marufuku kukata, kusafirisha, kufanya biashara au kutumia nguzo za miti.
Kualingana na sheria hiyo, nguzo ni mti ambao haujaukomaa, wenye kipenyo cha chini ya sentimita 20, na kipimo cha mita 1.30 kutoka ardhini. Hata hivyo, nguzo zinaweza kuvunwa, kusafirishwa, kuuzwa au kutumika chini ya kibali kilichotolewa kwa sababu maalumu, imeeleza.
Anatozwa faini ya sawa na mara mbili ya thamani ya nguzo zinazopatikana katika milki yake.
Sheria hii ni tofauti na pendekezo la awali ambalo lilijumuisha kutoza faini ya kiutawala ya dola 74.571 kwa mtu anayefanya biashara ya nguzo. Wakati huo huo, nguzo zinazohusika zinakamatwa na kukabidhiwa kwa mamlaka zilizo karibu na eneo la kukamatwa ili kuzitumia kwa maslahi ya umma.