Huku Rwanda ikijitayarisha kwa uchaguz mkuu Julai 2024, serikali imependekeza bunge kuidhinisha mabadiliko kadhaa katika Tume ya Uchaguzi.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Rwanda ilianzishwa mwaka 2000 kwa sheria ya Novemba 28, 2000, inayohusiana na utendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Sheria hii baadaye ilifutwa na sheria ya Disemba 24, 2005, ambayo imerekebishwa na kukamilishwa mara mbili - kwanza mnamo 2010, na mnamo 2013, kulingana na maelezo ya muswada huo.
Kwa mujibu wa sheria ya sasa, Baraza la Makamishna wa Tume liliundwa na wajumbe saba ambao walikuwa wakifanya kazi kwa njia zisizo za kudumu, isipokuwa miezi miwili kabla ya tarehe ya kupiga kura ambapo walipaswa kuitumikia tume kwa misingi ya kudumu kwa ajili ya ufuatiliaji mzuri wa mchakato wa uchaguzi.
Mapendekezo mapya ni kuwa makamishna watafanya kazi muda wote ili waweze kutimiza dhamira yao kwa ujumla.
Chini ya muswada huo, majukumu mahususi ya Tume yamependekezwa kuongezwa ambayo hayakujumuishwa hapo awali.
Kwa mfano, majukumu ya rais wa Tume yamependekezwa kuongezwa na kuiwakilisha Tume ndani na nje ya nchi, kuwa msemaji wa Tume, na kuwasilisha mpango kazi na taarifa za shughuli na hata taarifa za uchaguzi mkuu kwa husika.
Katika sheria iliyopo, hakuna nafasi ya Naibu Katibu Mtendaji. Hii imependekezwa kuongezwa.
Pendekezo hilo pia linataka sheria ya sasa kuunganishwa na katiba ya Rwanda.
Inapendekeza kwa mfano kama ilivyo kwa makamishna wengine wa Tume nyingine zinazotolewa na katiba ya taifa, kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi hafai kuwa na hatia ya uhalifu wa mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya ubinadamu, na awe hajawahi kuhukumiwa kifungo cha zaidi ya miezi sita.
Pia inapendekeza kuwa kamishna asiwe amewahi kuwa na nafasi ya uongozi katika taasisi za umma au binafsi.