Bunge ya Rwanda inapendekeza kuwe na utaratibu ya wanaotaka kuoana kukubaliana ni mali gani watagawana kabla ya ndoa / Picha: AP

Bunge ya Rwanda inajadili muswada ambao utawawezesha wanaotaka kuoana kupata haki ya kuchagua ni sehemu gani ya mali zao watakusanya pamoja au kutenganisha.

Hii wanafaa kukubaliana mapema kabla ya ndoa kufungwa, alisema Waziri wa Jinsia na Familia nchini Rwanda, Valentine Uwamariya akiwa bungeni.

Uwamariya anaelezea kuwa kuna taratibu tatu za mali katika ndoa.

Kuna ile inayohitaji mali kujumuishwa , ambayo ni mkataba ambao wanandoa huchagua umiliki wa pamoja wa mali zao zote.

Pia kuna mali ambayo washirika huchangia kila kitu wanachojenga kutoka siku ya harusi yao.

Ya tatu ni mgawanyo wa mali unaomaanisha mgawanyo kamili wa mali husika za wenye ndoa, bila usawazisho wowote wa faida iliyopatikana pindi ndoa yao inaisha.

Mswada huu ulio bungeni unadai kuwa, aina hizi tatu za taratibu za ndoa haziwapi wenzi watarajiwa chaguo la kubuni mfumo wao wenyewe kama ilivyo katika mikataba yote.

“Inawezekana kati ya mali tutakayomiliki kwa pamoja tunaweza kumiliki kwa pamoja sehemu yake katika ndoa, labda kuna mali ambayo mmoja wa washirika anagawana na wanafamilia wake, kwa mfano. Kisha, wanaweza kukubali kwamba mali kama hiyo haihesabiwi katika mali wanayoenda kukusanya,” alisema.

Mbali na kukubaliana kuhusu mali wanayokusanya, na kile wanachotenganisha baada ya ndoa chini ya utawala mpya,muswada huu unapendekeza wapenzi kukubaliana nini kitafanyika katika kesi ya talaka.

Hii itahusisha jinsi watakavyogawana mali inayomilikiwa kwa pamoja, au jinsi mali zingine zitakavyothibitiwa wakati mmoja wao anapokufa.

TRT Afrika