Serikali ya Rwanda inataka kupendekeza adhabu kali zaidi chini ya rasimu ya sheria mpya kuhusu uchimbaji madini na uchimbaji mawe ili kudhibiti biashara haramu ya madini.
Kwa miaka sita iliyopita, shughuli za uchimbaji madini zilifanywa chini ya sheria ya 2018 lakini imelaumiwa kwa kuwa na adhabu hafifu.
"Adhabu katika sheria zilikuwa nyepesi kiasi kwamba watu waliokuwa wakifanya makosa katika sekta hii ya madini na uchimbaji hawakuziogopa kwa sababu hazikuwa za kuzuia, ukilinganisha na thamani ya faida wanayopata katika sekta hii, au kile walichoweza kupata na kuzalisha iwapo wamefanya makosa,” Uwizeye alisema.
Kulingana na pendekezo ya sheria mpya, mtu anayemiliki madini yaliyochimbwa kinyume cha sheria ana hatia.
Hivyo atawajibika kwa adhabu ya kifungo kisichopungua miaka miwili lakini kisichozidi miaka mitano, na faini isiyopungua zaidi ya dola za kimarekani 23,000 (Rwf30 milion) na isiyozidi dola za kimarekani 46,000 (Rwf60 milioni) au moja ya adhabu hizi.
Pia inapendekeza kuwa mtu anayeruhusu shughuli ya uchimbaji madini kwenye ardhi yake kwa mtu asiye na leseni apate adhabu ya kifungo kisichopungua mwaka mmoja lakini kisichozidi miaka miwili, na faini isiyopungua zaidi ya dola za Marekani 19,000 (Rwf25 milioni) lakini isiyozidi dola za Marekani 30,000 (Rwf50 milioni) au moja ya adhabu hizi.
Iwapo mtu atakamatwa na madini bila uthibitisho wa asili yake, atatozwa faini sawa na asilimia 10 ya thamani ya madini hayo, na madini hayo kuchukuliwa na serikali.
Inapendekeza pia kuwa mtu mwenye leseni ambaye atashindwa kukarabati, kurejesha visima na kuchimba visima, kupanda miti, kuondoa majengo na kusawazisha sehemu yoyote iliyoathiriwa na uchunguzi au shughuli za uchimbaji madini, atakuwa na hatia.
Mtu huyo au kampuni hiyo itatozwa faini isiyopungua zaidi ya dola za Marekani 3800 (Rwf5 milioni) lakini isiyozidi zaidi ya dola za Marekani 7600 (Rwf10 milioni).
Muswada unapendekeza kipengele kipya kwa sheria.
Inaomba kuwa sheria ipitishe kuwa mtu anayefanya biashara ya madini yanayochimbwa kwa njia isiyo halali ana hatia. Atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha zaidi ya miaka mitano lakini isiyozidi miaka 10, na faini isiyopungua zaidi ya dola za Marekani 46,000 ( RW60 Milioni) lakini isiyozidi zaidi ya dola za Marekani 93,000 (Rwf120 milioni) au moja ya adhabu hizi.
Mapato ya mauzo ya nje ya madini ya Rwanda yalipanda kwa asilimia 43 hadi zaidi ya dola bilioni 1.1 (takriban Rwf1.4 trilioni) mwaka 2023, kutoka dola milioni 772 zilizorekodiwa mwaka 2022.
Lengo la nchi hiyo ni kuzalisha dola bilioni 1.5 ifikapo mwisho wa 2024, kulingana na Bodi ya Migodi, Petroli na Gesi ya Rwanda.