Rwanda inaadhimisha siku ya ukombozi  / Picha: Getty Images

Tarehe 4 Julai , Rwanda inaadhimisha 'Kwibohora', ambayo pia inajulikana kama siku ya ukombozi Rwanda.

Wananchi wa Rwanda duniani kote wanakumbuka wakati nchi yao ilipokombolewa kutoka kwa tawala zilizoingiza nchi hiyo katika mgawanyiko, ambao ulifikia kilele cha mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi mwaka 1994.

Zaidi ya Watutsi milioni moja waliuawa kati ya Aprili na mapema Julai mwaka huo.

"Tunasherehekea kuzaliwa upya kwa nchi yetu baada ya wanajeshi wa RPA kukomesha mauaji ya Kimbari dhidi ya Watutsi," serikali ya Rwanda imesema katika mtandawo wake wa Twitter.

"Tunathamini usalama uliohakikishwa, utu uliorejeshwa na matumaini yaliyorejeshwa. Pamoja tunafanikiwa," imeongezea.

Rwanda ilikumbwa na vita vya ndani kati ya wanajeshi wa Rwanda wakati huo chini ya uongoiz wa Juvénal Habyarimana , wakiwakilisha serikali ya nchi hiyo na waasi wa Rwandan Patriotic Front (RPF) kuanzia tarehe 1 Oktoba 1990 hadi 18 Julai 1994.

Vita hivyo vilitokana na mzozo wa muda mrefu kati ya makundi ya kikabila ya Wahutu na Watutsi nchini humo.

Vita vilianza tarehe 1 Oktoba 1990 wakati RPF ilipovamia Kaskazini-Mashariki mwa Rwanda, na hatimaye kuingia.

Baada ya miezi ya vita, RPF, chini ya Paul Kagame illikomboa mji mkuu , Kigali. wanajeshi wa RPF walilishinda nguvu Jeshi la Rwanda na kukomboa Kigali tarehe 4 Julai.

TRT Afrika