Nchini Nigeria wengi wanatumia sana sarafu za Crypto/ Picha: Reuters 

Benki ya Kitaifa ya Rwanda inapanga kuweka kanuni za matumizi na biashara ya sarafu ya crypto.

Gavana wa Benki Kuu ya Rwanda, John Rwangomba inatarajiwa kwamba, katika robo ya kwanza ya 2025, Benki Kuu itakuwa imekubaliana na Mamlaka ya Soko la Mtaji la Rwanda (CMA) kuhusu kanuni za sarafu ya hiyo.

Crypto ni aina ya sarafu ya kidijitali ambayo inaruhusu watu kufanya malipo moja kwa moja kupitia mfumo wa mtandaoni.

Hazina thamani iliyohalalishwa au ya asili, zinafaa tu kile ambacho watu wako tayari kuzilipia sokoni.

Hii ni tofauti na sarafu za kitaifa, ambazo hupata sehemu ya thamani yake kutokana na kupitishwa kisheria kama zabuni halali.

Rwangomba amesema sarafu za kidijitali ni tete sana kwani wakati mwingine thamani yake hupanda sana, wakati mwingine husuka.

"Ni sarafu ambazo watu hujihusisha nazo na waliobahatika kupata faida kutoka kwao na kuwa mamilionea kwa muda mfupi, na wasio na bahati hata hupoteza walichokuwa nacho," Rwangombwa alisema.

Gavana ameongezea kuwa kutokuwepo kwa sheria za kimataifa zinazodhibiti sarafu za crypto ni changanmoto.

"Tunachofanya, kwa kushirikiana na Mamlaka ya Soko la Mitaji, kwa kuzingatia kile kinachofanyika katika ngazi ya kimataifa, ni kuweka kanuni zinazosimamia kile tunachokiita mali halisi ambayo inaweza kuuzwa katika nchi yetu," alisema.

Nchi jirani za Kenya na Tanzania bado hazijahusisha sarafu za Crpto kama sarafu halali za biashara.

TRT Afrika