Rwanda iko tayari kuandaa Mkutano Mkuu wa FIA kwa mwaka 2024, Rais wa Chama cha Mbio za Magari nchini humo, Christian Gakwaya amesema.
Mkutano huo unatarajiwa kufanyika jijini Kigali kuanzia Disemba 8 hadi 13, kulingana na Gakwaya.
Mkutano Mkuu wa mbio za ‘Formula One’ ni kipindi muhimu katika kalenda ya FIA.
“Mkutano huu unadhihirisha utayari wetu na hakuna namna nyingine ya kuwa tayari kuwa mwenyeji wa mbio hizi maarufu duniani,” Gakwaya alisema.
“Tunazidi kukua na tutafanya mambo mazuri zaidi hapo baadaye, ni kitu kikubwa sana kuileta dunia yote Kigali,” aliongeza.
Agosti mwaka huu, Afisa Mtendaji Mkuu wa Formula One Stefano Domenicali alisema kuwa mkutano huo utafanyika nchini Rwanda kuangalia mpango wa nchi hiyo kuwa mwenyeji wa mbio hizo za magari yenye kasi na ghali zaidi duniani.