Rwanda imesema iko tayari kuanza kuuza maji maji ya damu au utegili kwa nchi za nje.
Uuzaji wa plasma umetolewa katika Agizo la Waziri la Julai 11, 2024, inayohusu njia za matumizi ya mwili wa binadamu, viungo, tishu, seli na bidhaa za mwili wa binadamu, ambayo ilichapishwa katika Gazeti Rasmi, Julai 12.
Inafafanua plasma kama sehemu ya kioevu cha njano-nyepesi ya damu ambayo inabaki baada ya seli nyekundu za damu, seli nyeupe za damu, na vipengele vyengine vya seli kuondolewa katika damu.
Kulingana na agizo la mawaziri, bidhaa za mwili wa binadamu ambazo zinaweza kuuzwa ni plasma inayotolewa katika damu. Inasema kwamba bei ya plasma ni angalau $50 kwa lita.
"Ukizingatia takribani asilimia 5 ya lita 40,000 kwa mwaka, utagundua kuwa takriban lita 2,000 zinatumika. Hii inamaanisha kuwa lita 38,000 za plasma zinapotea," Dkt. Muyombo amesema.
Plasma inatumika kuhudumia wagonjwa wanaokabiliwa na upungufu wa maji mwilini, na wale wanaougua magonjwa makubwa kama saratani na malaria, pamoja na kutokwa na damu nyingi ambazo hupunguza kiwango cha damu, kwa mujibu wa taarifa kutoka Rwanda Biomedical Center (RBC).
Takwimu kutoka Kituo cha Afya cha Rwanda (RBC) zinaonyesha kwamba ugavi wa damu katika hospitali umefikia asilimia 99.42 kufikia mwaka wa 2022.
Pia, RBC inasema kwamba uniti 78,838 zilitolewa mwaka 2022, ambapo uniti 21,482 zilichangwa na vijana kati ya umri ya miaka 18 na 25.
Mtaalamu huyo amesema Rwanda inashirikiana na kampuni za kigeni kuhakikisha kuwa angalau plasma hii inayosafirishwa inaagizwa tena kama bidhaa iliyokamilika ambayo inaweza kutolewa kwa njia ya dawa kwa wagonjwa nchini Rwanda.