Takriban waomba hifadhi 24,000 walipaswa kuhamishiwa Rwanda, huku Uingereza ikiripotiwa kuilipa Rwanda takriban dola milioni 176 kwa uhamisho huo Juni 2022. / Picha: TRT Afrika

Serikali ya Rwanda ilisema Jumanne kwamba mkataba wake wenye utata wa wahamiaji na Uingereza haukuweka wazi kurejeshwa kwa fedha, kufuatia uamuzi wa serikali mpya ya Uingereza kufuta mpango huo.

"Mkataba tuliotia saini haukuweka bayana kwamba tunapaswa kurejesha pesa. Hili liwe wazi, kulipa pesa hizo kamwe haikuwa sehemu ya makubaliano," naibu msemaji wa serikali Alain Mukuralinda aliambia televisheni ya taifa.

Takriban waomba hifadhi 24,000 walitakiwa kuhamishiwa Rwanda, huku Uingereza ikiripotiwa kuilipa Rwanda takriban dola milioni 176 kwa uhamisho huo Juni 2022.

Uingereza pia ilipaswa kulipa $15,100 kwa kila mtu wa ziada aliyepelekwa Rwanda.

Uhamiaji halisi

Uingereza inaruhusu maombi ya hifadhi, aina ya ulinzi ambayo huwezesha mtu kusalia nchini bila kufukuzwa.

Uingereza inatarajia kupunguza idadi ya wanaotafuta hifadhi hadi chini ya 100,000 kila mwaka. Serikali ilisema kuwa mnamo 2022 pekee, kulikuwa na wahamiaji 606,000.

TRT Afrika