Wagombeaji watatu wanasaka kiti cha Urais katika uchaguzi wa Rwanda  utakaofanyika  kutoka tarehe14 hadi 16 Julai 2024 / Picha: Reuters

Tume ya uchaguzi nchini Rwanda ilitangaza kuwa tarehe 13 Julai, kuwa siku ya mwisho za kampeni za wagombeaji wa uchaguzi mkuu nchini humo.

Uchaguzi wa urais na wabunge utafanyika tarehe 14 hadi 16 Julai 2024.

Rais wa sasa Paul Kagame atakutana na wapinzani wawili wanaogombea kiti cha urais nchini humo.

Kampeni za rais kagame zimeonekana kuvutia watu wengi zaidi ya wagombeaji wale wengine.

Waatalamu wa kisiasa wanasema kuwa rais ana bahati ya kutumia rasilimali za serikali kufika meneo yote ya nchi kwa urahisi, ilhali wale wengine wanategemea tu rasilimali walizopata kutoka kwa tume ya uchaguzi.

Paul Kagame mwenye miaka 66, alisaidia kuongoza vuguvugu la waasi  ambalo lilokomesha mauaji ya kimbari ya 1994 nchini Rwanda, amehudumu kama rais tangu 2000/ Picha : AFP 

Wagombea wawili wengine ni Frank Habineza wa chama cha Democratic Green Party na Philippe Mpayimana, mfanyakazi katika Wizara ya Umoja wa Kitaifa na Ushirikiano wa Kiraia.

Walichuana na Kagame mwaka 2017.

Wagombeaji wanane walitaka nafasi ya kushiriki kwenye kinyagariko

Wadadisi wa kisiasa wanadai kuwa Rais wa Rwanda Paul Kagame, anatarajiwa kurejea kwa muhula wa nne madarakani, katika uchaguzi utakaofanyika Jumatatu dhidi ya wagombea wawili wa upinzani ambao waliruhusiwa kuchuana naye, lakini wana matarajio madogo tu.

Kagame mwenye miaka 66, alisaidia kuongoza vuguvugu la waasi ambalo lilikomesha mauaji ya kimbari ya 1994 nchini Rwanda na amehudumu kama rais tangu 2000.

Anakabiliwa na wapinzani wawili tu kwa sababu wagombea wengine sita hawakuruhusiwa kugombea na tume ya uchaguzi ya serikali.

Victoria Ingabire ni mmoja wao

Wagombea wanane walikuwa wametuma maombi ya kugombea dhidi ya Kagame, lakini ni wawili pekee waliobaki kwenye orodha ya mwisho iliyoidhinishwa na tume ya uchaguzi.

Wagombea wawili wengine ni Frank Habineza na Philippe Mpayimana/ picha: AFP

Wengine, wakiwemo wakosoaji wengi wa Kagame, walibatilishwa kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na makosa ya awali ya uhalifu.

Kati yao ni Victoria Ingabire.

Machi 2023 mahakama nchini Rwanda ilizuia juhudi za kiongozi mashuhuri wa upinzani Victoire Ingabire kugombea kiti cha urais na kukataa kuondoa marufuku ya kumuidhinisha yeye kuwania kiti hicho. Ingabire aliachiliwa mnamo 2018 baada ya kukaa miaka minane gerezani kwa kutishia usalama wa serikali na "kutoheshimu" mauaji ya kimbari ya 1994.

Nchini Rwanda, watu ambao wamefungwa kwa zaidi ya miezi sita wamezuiwa kushiriki katika uchaguzi.

Machi 2023 mahakama nchini Rwanda ilizuia juhudi za kiongozi mashuhuri wa upinzani Victoire Ingabire kugombea kiti cha urais. /Picha: AFP

Ingabire alisema uamuzi wa mahakama ulikuwa wa kisiasa.

Mwaka 2010, Ingabire alirejea kutoka uhamishoni Uholanzi, ili kushiriki katika uchaguzi wa rais wa mwaka huo.

Lakini alikamatwa, na kuzuiwa kugombea na baadaye akahukumiwa kifungo cha miaka 15 jela.

Akiwa wa kabila la Wahutu, aliingia matatani kwa kuhoji ni kwa nini ukumbusho rasmi wa Rwanda wa mauaji ya halaiki ya 1994 haukujumuisha Mhutu yeyote.

Mwaka wa 2018, Ingabire alisamehewa na serikali na akaunda chama cha upinzani cha Dalfa-Umurinzi.

TRT Afrika