Uchaguzi wa 2024 ni kura ya pili ya urais kufanywa chini ya usimamizi kamili wa mamlaka huru ya uchaguzi tangu uchaguzi wa 2019. / Picha: AA

Rais wa sasa wa Algeria Abdelmadjid Tebboune ameshinda muhula wake wa pili wa urais wa miaka mitano katika uchaguzi wa mapema uliofanyika Jumamosi, mamlaka ya uchaguzi nchini humo ilitangaza Jumapili.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Mohamed Charfi, mkuu wa Mamlaka Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (ANIE), alitangaza kuwa Tebboune alishinda kwa 94.65% ya kura.

Aliongeza kuwa mgombea Abdelali Hassani Cherif, kiongozi wa Movement for Society and Peace (chama kikubwa zaidi cha Kiislamu), alishika nafasi ya pili kwa kupata asilimia 3.17 ya kura.

Youcef Aouchiche, katibu wa kwanza wa kitaifa wa Socialist Forces Front (chama kikongwe zaidi cha upinzani/chama cha mrengo wa kushoto), aliibuka wa tatu na wa mwisho kwa 2.16% ya kura.

Mrejeleo

Charfi aliripoti kuwa kura zilizopigwa kwa wagombea hao watatu zilikuwa jumla ya milioni 5.7 kati ya zaidi ya wapiga kura milioni 24 waliojiandikisha.

Mamlaka ya uchaguzi inatarajiwa kupeleka mara moja rekodi za kuhesabu kura kwa Mahakama ya Kikatiba, ambayo itakuwa na hadi saa 48 kukagua rufaa zozote zinazowezekana, huku matokeo ya mwisho yakitangazwa ndani ya siku kumi.

Mapema Jumapili, Charfi alisema kuwa idadi ya wapiga kura wakati wa kufunga vituo vya kupigia kura saa nane mchana Jumamosi (1900GMT) ndani ya Algeria ilikuwa 48.03%.

Idadi hii ilipita idadi ya mwisho ya wapigakura waliojitokeza kwenye uchaguzi wa urais mwaka wa 2019, ambayo ilikuwa 39.88%.

Huu ni uchaguzi wa pili wa urais kufanywa chini ya usimamizi kamili wa mamlaka huru ya uchaguzi tangu uchaguzi wa 2019, ilhali hapo awali, chaguzi zilisimamiwa na Wizara ya Mambo ya Ndani.

TRT Afrika