Polisi nchini Rwanda imetoa tahadahari kwa waendesha pikipiki kuwa makini zaidi kwani ajali zinayohusishwa na pikipiki zimeongezeka.
Ripoti ya polisi inaonyesha kuwa katika kipindi cha miezi sita iliyopita, jijini Kigali, limeripoti zaidi ya ajali 890 zilizohusishwa na pikipiki.
Katika kikao na maelfu ya madereva wa pikipiki jijini Kigali, Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi anayesimamia Operesheni, Vincent Sano, aliwataka madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali.
"Pikipiki nyingi zinakamatwa na kupigwa faini kubwa ambazo hazijalipwa kutokana na uvunjaji wao wa sheria unaoendelea," Sano alisema.
Ajali hizi kimsingi zinachangiwa na madereva walevi, zimezua wasiwasi kuhusu usalama barabarani jijini, kulingana na polisi.
Mbali na suala hilo, zaidi ya pikipiki 1,100 zimekamatwa na polisi kutokana na ukiukwaji mbalimbali. Wengine wanalaumiwa kwa kujaribu kuficha namba za leseni.