Paul Kagame wa Rwanda awafuta kazi zaidi ya maafisa 200 wa jeshi

Paul Kagame wa Rwanda awafuta kazi zaidi ya maafisa 200 wa jeshi

Taarifa kutoka jeshi la taifa RDF haijatoa sababu za maafisa hao kuachishwa kazi.
Rais Paul Kagame amewafuta kazi zaidi ya maafisa 200 wa jeshi/ Picha: Ikulu ya Rwanda.

Rais wa Rwanda Paul Kagame, ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF), amemfuta kazi Meja Jenerali Martin Nzaramba kutoka jeshini, hii ni kwa mujibu wa taarifa ya 30 Agosti 2024 kutoka RDF.

"Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Rwanda na Amiri Jeshi wa RDF amewafukuza kazi Meja Jenerali Martin Nzaramba, Kanali Dkt. Etienne Uwimana na maafisa wengine wakubwa na wadogo 19," taarifa ya jeshi la RDF imesema.

Meja Jenerali Uwimana alikuwa daktari katika Hospitali ya Jeshi la Rwanda ambapo alikuwa msimamizi wa idara ya X-ray.

Nzaramba, Mkuu wa zamani wa Kituo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Nasho, alikuwa amestaafu kutoka jeshini Agosti 2023.

Hapo awali aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo ya Kupambana cha Gabiro Gabiro kilichoko Wilaya ya Gatsibo.

Taarifa ya Jeshi la RDF pia inasema Rais Kagame pia aliidhinisha kufutwa na kubatilishwa kwa kandarasi za vyeo vyengine 195 kutoka kwa RDF.

29 Agosti 2024 Rais Kagame alifanya mkutano na viongozi wa jeshi, ambapo Ikulu ilisema walijadili masuala ya amani na usalama ya Rwanda.

TRT Afrika