Parachichi ilivuna zaidi ya dola milioni 11 katika mapato ya zaidi ya dola milioni 34.7 ambayo Rwanda ilijipatia kutoka kwa mauzo ya matunda aina 10 / Picha: AP

Ripoti ya Taasisi ya Taifa ya Takwimu ya Rwanda imeonyesha kuwa Rwanda inapata mapato zaidi kutokana na mauzo ya matunda nje ya nchi.

Mapato ya Rwanda kutokana na mauzo ya matunda yaliongezeka hadi dola milioni 34.7 milioni (zaidi ya Rwf52.6 bilioni) katika mwaka wa fedha wa 2023/2024, ripoti mpya inaonyesha.

Hili ni ongezeko kutoka dola milioni 19 ya mwaka uliopita.

Ripoti hiyo iliyotolewa tarehe 31 Disemba inaonyesha kuwa zaidi ya aina 10 za matunda na bidhaa zinazohusiana zilichangia ufanisi wa mauzo ya nje, huku parachichi zikizalisha theluthi moja ya mapato.

Mauzo ya parachichi

Parachichi ilivuna zaidi ya dola milioni 11.

Mwaka uliopita wa 2022/2023 Rwanda ilipata zaidi ya dola milioni 6.3 kutoka kwa mauzo ya parachichi.

Bodi ya Kitaifa ya Rwanda ya Maendeleo ya Mauzo ya Nje ya Kilimo (NAEB) inaonyesha kuwa Parachichi, ambayo inachukuliwa kuwa mojawapo ya bidhaa mpya za mauzo ya nje nchini na NAEB, yameonekana kuongezeka kwa kiasi na mapato.

Zao hili lilivutia mapato ya zaidi ya dola $840,570 mwaka 2019/2020

Baadhi ya aina nyengine za matunda zinazoongoza kwa ongezeko la 2024 ni pamoja na machungwa, ambayo yalichangia zaidi ya dola milioni 3.9, ndizi mbivu zaidi ya dola milioni 1.6 milioni, na maembe zaidi ya dola milioni1.5 milioni.

Rwanda ilianza usafirishaji wa parachichi kwa mara ya kwanza Novemba 2022 ilipotuma shehena Dubai, na ya pili Rotterdam huko Uholanzi, mnamo Novemba 2023.

Januari 2024, ilifanya usafirishaji wa baharini wa kontena lililokuwa na jokofu lenye tani 22.5 za aina ya parachichi aina ya Fuerte na Hass hadi Dubai, huku ikiendelea na majaribio ya kuuza matunda hayo ikitumia njia mbadala mbali na usafirishaji wa anga.

TRT Afrika