Watu wanafanya kazi katika uharibifu katika jiji la kihistoria la Marrakech, kufuatia tetemeko kubwa la ardhi huko Morocco / Picha: Reuters

Idadi ya vifo nchini Morocco iliongezeka hadi 1037, huku mamia ya wengine wakijeruhiwa, wizara ya mambo ya ndani imesema katika ripoti yake ya hivi punde.

Lakini idadi kamili haikujulikana kwani waokoaji walihangaika Jumamosi asubuhi kupita kwenye barabara zilizojaa mawe zinazoelekea kwenye vijiji vilivyoathirika zaidi.

Tetemeko hilo lisilo la kawaida lenye uzito 7 katika vipimmoi vya Richter, lilitokea katika mikoa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mikoa ya Al Haous na Marrakesh, pamoja na miji ya Ouarzazate, Azilal, Chichaoua na Taroudant.

Tetemeko la ukubwa wa 6.8 ndilo lililokuwa baya zaidi kuikumba Morocco katika kipindi cha miaka 120, na liliangusha majengo na kuta katika miji ya kale iliyotengenezwa kwa mawe na uashi ambayo haikuundwa kustahimili matetemeko.

Viongozi wa dunia walijitolea kutuma wahudumu wa misaada au waokoaji huku rambirambi zikimiminika kutoka nchi za Ulaya, mkutano mkuu wa Kundi la 20 nchini India, nchi za Afrika, na Mashariki ya Kati.

Mtazamo wa jumla wa uharibifu katika mji wa kihistoria wa Marrakech, kufuatia tetemeko kubwa la ardhi huko Morocco/ Picha :

Wakala wa Jiolojia wa Marekani umesema tetemeko hilo lilikuwa na ukubwa wa awali wa 6.8 lilipopiga saa 11:11 jioni. (2211 GMT), kwa mtetemeko uliochukua sekunde kadhaa. Shirika la Umoja wa Mataifa liliripoti mshtuko wa nyuma wa kipimo cha 4.9 dakika 19 baadaye.

TRT Afrika