Hivi karibuni, Nigeria iliruhusu sekta binafsi kuingia kwenye huduma za uzalishaji umeme./Picha: Reuters  

Na Abdulwasiu Hassan

Katika kipindi cha zaidi ya wiki moja, sehemu kubwa ya Nigeria ilikuwa kwenye giza nene baada ya washukiwa wa ugaidi kuharibu miondombinu ya usafirishaji wa nishati hiyo muhimu.

Tukio hili sio tu lilisitisha shughuli za kibiashara katika eneo hilo, bali pia lilidhihirisha mambo ya kawaida yatokeayo nchini humo.

Namba huwa hazidanganyi

Takwimu zinaonesha kuwa Nigeria inashika nafasi ya kumi kwa hifadhi kubwa ya mafuta duniani na nafasi ya nane kuwa na hifadhi kubwa ya gesi ulimwenguni.

Imekuwa ni kawaida kwa watu kutumia jenereta zinazotumia simu pale umeme unapokatika nchini Nigeria./Picha: Reuters

Kutokana na takwimu hizo, ni vigumu kuelewa wala kuamini kwanini sehemu kubwa ya Nigeria bado inakabiliana na tatizo la umeme.

Kama hiyo haitoshi, Nigeria bado inakabiliana na changamoto ya kutoa huduma sahihi ya nishati ya umeme kwa raia wake.

Kulingana na Mkurugenzi Mkuu wa Uendeshaji kutoka Benki ya Dunia, Anna Bjerde, Nigeria ina idadi kubwa ya watu wasio na huduma ya umeme kati ya mataifa yote yanayokabiliana na shida kama hiyo.

"Zaidi ya watu milioni 85 wanakabiliwa na shida ya umeme," aliandika mtandaoni. "Ni jambo la kushangaza na kushtusha kuwa Nigerai, nchi yenye nishati nyingi bado inakabiliana na shida kama hii."

Ahadi hewa

Vizazi vingi vimeshuhudia tatizo hili licha za ahadi zisizoisha za kumaliza changamoto hiyo kutoka kwa serikali.

Shirika la uzalishaji wa umeme nchini Nigeria limekuwa likiripoti uharibifu wa miundombinu yake./Picha: X/TCN

Baadhi ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali katika kukabiliana na tatizo la upatikanaji wa umeme hafifu kote nchini ni pamoja na uwekezaji katika mitambo ya maji, gesi na nishati ya jua.

Mbali na uwekezaji huo, nchi hiyo imeshuhudia mageuzi mbalimbali yanayolenga kuifanya sekta hiyo kuwa na ufanisi zaidi.

Kuanzia ubinafsishaji wa makampuni ya usambazaji umeme hadi kupunguzwa kwa udhibiti kamili wa sekta ili kuvutia uwekezaji wa kigeni, hakuna kitu kilichofanya kazi kikamilifu.

"Ili sekta hii ifufuliwe, serikali lazima itumie walau dola bilioni 10 kila mwaka katika kipindi cha miaka 10 ijayo. Miundombinu inahitajika kwa utulivu wa sekta hiyo, lakini serikali haiwezi kumudu matumizi hayo," waziri wa nishati wa Nigeria Adebayo Adelabu aliambia kamati ya bunge.

"Kwa hiyo, lazima tuifanye sekta iwe ya kuvutia kupitia bei za kibiashara," alifafanua.

Wateja wa daraja A wanapaswa kubeba mzigo wa bei shindani, wanasema kuwa kutoza ada haileti maana huku usambazaji wa nishati umepungua.

Kushindwa kufanya kazi kwa gridi

Nigeria inazalisha kiasi cha megawati 6,000 za umeme kwa watu milioni 200, ambayo ni tofauti na Afrika Kusini ambayo inazalisha megawati 48,000 kwa watu milioni 60.

Waziri wa Nishati nchini Adebayo Adelabu./Picha: @BayoAdelabu

Wataalamu wanasema kuwa kukatika mara kwa mara kwa umeme nchini humo kunatokana na uzalishaji mdogo na usambazaji wa umeme.

Alitaja uharibifu wa njia za kusambaza umeme na miundombinu ya zamani, ikiwemo transfoma na vifaa vingine vya gridi ya taifa, kuwa ndiyo unaosababisha adha ya sekta ya umeme.

"Takwimu zinaonesha kuwa kuanzia Januari 2024 hadi sasa, minara 66 ya kusambaza umeme iliharibiwa kote Nigeria," alisema Dkt Ibrahim.

Suluhu

Je, kuna tumaini lolote la kupata suluhisho wakati serikali inasubiria uwekezaji kwenye sekta ya nishati?

Bjerde anaamini kuwa ni vyema nchi hiyo ikawekeza kwenye nishati jadidifu kama suluhisho sahihi la tatizo hilo.

Watu wataanza matumizi ya majenereta wakati umeme utakapotengemaa./Photo: Reuters

"Serikali mbalimbali zinahitaji kuwekeza katika mapinduzi ya nishati safi kupitia mageuzi na mifumo thabiti ya sera na udhibiti," alisema.

Kwa kuwa huduma ya uzalishaji umeme nchini Nigeria haidhibitiwi kwa kiwango kikubwa, kikwazo cha udhibiti bado kiko njiani.

Hata hivyo, kwa wataalamu wa masuala ya nishati kama vile Dk Ibrahim, suluhisho pekee ni zaidi ya mapinduzi safi ya nishati. "Kuna haja ya uboreshaji wa gridi ya taifa, uboreshaji wa matengenezo, na ugatuzii wa uzalishaji wa umeme kupitia uwekezaji wa nishati mbadala," aliiambia TRT Afrika.

"Vyanzo vinavyoweza kurejeshwa kama vile jua, upepo, na hydro, ambavyo vinapatikana kwa wingi kaskazini, vinaweza kupunguza shinikizo kwenye gridi ya taifa na kuboresha kutegemewa."

Zaidi ya Wainigeria wasio na umeme watakuwa na imani kuwa juhudi mbalimbali zitafanyika ili kupata suluhu ya kudumu.

TRT Afrika