Jeshi la Nigeria limewaua watu 56 wenye silaha kote nchini humo ndani ya wiki mbili, taarifa kutoka makao makuu ya ulinzi ya Nigeria imesema.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Habari katika Makao Makuu ya Ulinzi Nigeria, Meja Jenerali Musa Danmadami, inasema kuwa wanajeshi hao pia waliwakamata watu 36 wenye silaha katika eneo la Kaskazini-Magharibi mwa nchi hiyo.
Katika miaka ya hivi karibuni jeshi la Nigeria limelazimika kuongeza matukio ya utekajinyara Kaskazini-Magharibi kuwa sehemu ya vitisho vya usalama wa ndani ukiweka pembeni vita yao ya kuwasaka Boko Haram.
Danmadami aliongeza kuwa wanajeshi hao waliwa kamata wasambazaji wa vifaa kwa Boko Haram pamoja na kuwaokoa raia 119.
Taarifa hiyo ilisema wapiganaji 1,506 wa Boko Haram na familia zao walijisalimisha kwa wanajeshi wa Nigeria katika muda wa wiki mbili hizo.
Alisema Jeshi la Anga la Nigeria lilishambulia kwa mabomu maeneo ya Boko Haram katika majimbo ya Borno na Yobe Kaskazini Mashariki mwa nchi ambapo wapiganaji wengi waliuawa.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa watu 28 wenye silaha walikamatwa Kaskazini mwa Nigeria wakiwemo majambazi na wahalifu wa kisiasa.