Mamlaka ya Kitaifa ya Chakula na Dawa (NAFDAC) nchini Nigeria imetoa agizo la kutoa kwenye soko kundi la chupa za Sprite zinazosambazwa nchini humo kwa sababu zinaweza kuwa na chembechembe za sumu.
NAFDAC ilisema uchunguzi uligundua baadhi ya bidhaa hizo kuwa na uchafu baada ya malalamiko kutoka kwa watumiaji.
"Baada ya uchunguzi, katika hatua ya kununua na anwani ya muuzaji, zaidi ya kreti tano ya kundi lenye tatizo la chupa za Sprite zenye ujazo wa mililita 50 ziligundulika kuwa na chembechembe za uchafu," ilisema taarifa iliyotolewa Jumamosi lakini iliyotangazwa Jumatano kupitia mitandao wa kijamii.
Mamlaka husika hazijatoa maelezo kuhusu chembechembe hizo na madhara yake.
Kampuni ya Nigerian Bottling Company Limited katika kiwanda cha Abuja imeagizwa kutoa kwenye soko kundi hilo lenye tatizo. Kampuni hiyo bado haijatoa maoni kuhusu uamuzi huo.
Tahadhari
Wauzaji na watumiaji wamehimizwa kuchukua tahadhari ili kuepuka matumizi ya bidhaa zilizoathiriwa.
Mwezi wa Mei, msimamizi huyo alisema ulikuwa unachunguza chapa maarufu ya mihogo baada ya kuwa na kurudishwa tena kwenye soko nchini Malaysia na Taiwan ambako mamlaka zilisema waligundua kemikali inayoweza kusababisha saratani.