Makamu wa Rais nchini Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah, anaelekea kushinda kiti cha Urais wa nchi hiyo huku nusu ya kura zote zilizohesabiwa zikionesha kuwa yuko juu ya asilimia 50.
Matokeo kutoka majimbo 60 kati ya 121 yanaonesha kuwa Nandi-Ndaitwah kutoka chama tawala cha SWAPO akiongoza kwa asilimia 54.2 ya kura, akifuatiwa na Panduleni Itula kutoka chama cha IPC, akiwa amejikusanyia kura 27.6.
Bernadus Swartbooi wa chama cha IPM, yuko katika nafasi ya tatu akiwa na asilimia 6.3 ya kura zote, kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi ya Namibia siku ya Jumatatu.
McHenry Venaani wa chama cha PDM amejizolea asilimia 4.7 ya kura zote na kushika nafasi ya nne huku Job Amupanda kutoka AR, akiwa na kura asilimia 1.9 na kushika nafasi ya tano.