Mamlaka ya Hali ya Hewa ya Rwanda imeonya kuwa maeneo ya kusini-magharibi mwa nchi yataendelea kunyesha juu ya kiwango cha kawaida cha mvua hadi Januari 20, 2024.
"Athari zinazohusiana na mvua kubwa zinawezekana katika maeneo ya kusini-magharibi mwa nchi ambako mvua zinazoongezeka [kati ya milimita 60 na 120] zinatarajiwa," Mamalaka hiyo imesema.
"Athari zinazowezekana ni mafuriko, mmomonyoko wa udongo na maporomoko ya ardhi katika maeneo yanayokumbwa na mafuriko," imeongeza kusema Mamlaka hiyo.
Tayari madhara yameanza kuonekana
Januari tarehe 13, radi ilipiga kwenye Uwanja wa Gicumbi, na kuwaacha watu 10 wakiwa wamejeruhiwa. Pia iliharibu nyumba 14 na madarasa mawili pamoja na mazao katika eneo la Mbazi Wilaya ya Huye.
Januari tarehe 14, mvua kubwa iliharibu nyumba za watu 22 katika wilaya ya Nyamasheke ikiwa familia hizo zimelazimika kuhifadhiwa na majirani zao.
Mamlaka hiyo ya maandalizi na hatua za kukabiliana nazo zinapaswa kuwekwa ili kupunguza athari zinazoweza kusababishwa na mvua zinazotarajiwa.
Mwezi Mei mwaka 2023, mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa yalipelekea vifo vya zaidi ya watu 130 nchini Rwanda, Magharibi, Kaskazini na Kusini mwa Rwanda.