Mtoto wa afisa mkuu wa usalama anayemlinda Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amepatikana amefariki.
Warren Rhoode, mtoto wa Meja-Jenerali Wally Rhoode, alipatikana Ijumaa baada ya kutoweka kwa siku 12, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 31 alionekana mara ya mwisho Aprili 23 akiendesha gari lake aina ya Volkswagen Polo, eneo la Delft viungani mwa Cape Town.
Polisi wanachunguza madai kuwa aliuawa baada ya kutekwa nyara na watu wasiojulikana.
Mabaki ya Warren yalipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha Tygerberg huko Cape Town.
Shangazi wa marehemu, Anthula Messeur, alisema juhudi za kumtafuta zimeambulia patupu.
Msemaji wa Polisi wa Afrika Kusini Brigedia Athlenda Mathe alisema uchunguzi umeanza kuhusu hali ya kifo cha Warren.