Taarifa za kutekwa kwa Mahinini ambaye ni Frateri wa shirika la wamisionari wa Afrika (White Fathers) zimethibitishwa jana tarehe 7 Agosti na balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Benson Alfred Bana

Akizungumza na TRT Afrika Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Benson Alfred Bana, amethibitisha taarifa za kuachiwa huru mseminari huyo mzaliwa wa Kabanga mkoani Kigoma.

"Shukran nyingi kwa maombi ya wananchi na buheri, taarifa tumepata saa tisa alfajiri na waliachiliwa wakiwa na afya njema’’. Bana aliiambia TRT Afrika.

Balozi Bana ameishukuru serikali ya Tanzania pamoja na watu wa ulinzi Nigeria kwa kazi nzuri waliofanya ili kuwaokoa vijana waliotekwa. Aidha Bana alitoa shukrani zake kwa jimbo katoliki kwa ushirikiano kutoka nchi zote mbili.

Kwa mujibu wa Balozi Bana, Mahini ameachiwa huru na wenzake majira ya saa 9 alfajiri kwa saa za Nigeria wakiwa na afya njema kabisa.

Mahinini ambaye ni Frateri wa shirika la wamisionari wa Afrika (White Fathers) alitekwa nyara na watu wasiojulikana pamoja na mwenzake Padri Paul Sanogo raia wa Burkina Faso mnamo tarehe 3 Agosti mwaka huu.

TRT Afrika