Mkuu wa eneo lililokumbwa na ghasia nchini Ethiopia la Amhara, ambalo serikali ya shirikisho imeliweka chini ya hali ya hatari, amejiuzulu, kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyoripotiwa Ijumaa.
Bunge la Amhara "limekubali kujiuzulu kulikowasilishwa na rais wa eneo hilo, Dk. Yilkal Kefale, na kumteua Arega Kebede badala yake," bunge hilo lilisema katika taarifa iliyoripotiwa na shirika rasmi la Amhara Media Corporation.
Kujiuzulu siku ya Jumatano kulikuja baada ya bunge, linalojulikana kama Baraza la Mkoa, kujadili "hali ya sasa ya usalama ya mkoa", ilisema.
"Baada ya majadiliano ya pamoja yalifikiwa (juu ya haja) ya mageuzi thabiti," ilisema.
Vita vya Tigray
Mvutano katika eneo la kaskazini uliongezeka mwaka huu baada ya kumalizika kwa vita vibaya katika eneo jirani la Tigray ambavyo pia viliwahisisha wapiganaji kutoka Amhara.
Mnamo Aprili serikali ya shirikisho ilitangaza kuwa inavunja vikosi vya mkoa kote nchini.
Hatua hiyo ilizua maandamano ya wanaitaifa wa Amhara ambao walisema itadhoofisha eneo lao.
Mapigano yalizuka mapema mwezi Julai kati ya jeshi la taifa na wapiganaji wa eneo hilo, na kusababisha mamlaka mjini Addis Ababa tarehe 4 Agosti kutangaza hali ya hatari ya miezi sita.