NISS pia imekamilisha juhudi mbalimbali za kutatua matatizo ya kiusalama nchini Ethiopia. Picha: ENA

Idara ya Usalama wa Taifa ya Ethiopia (NISS) imetangaza kuwa watu hao ni miongoni mwa zaidi ya washukiwa 3,000 waliokamatwa kwa kujihusisha na vikundi vya kigaidi, utakatishaji fedha na ufisadi.

Idara hiyo, imetoa taarifa hiyo wakati wa tathmini yake ya kila mwaka juu ya utendakazi wake pamoja na maelekezo ya shughuli za siku zijazo huku ikisema kuwa imewakamata wanachama wa Al-shabaab na Daesh na kubatilisha mashambulizi ya kigaidi yaliyolenga raia wasio na hatia.

Aidha, Ethiopia imeongeza kuwa operesheni hiyo imefanikiwa kwa ushirikiano na taasisi za ndani na za kigeni zilizofanya juhudi nyingi kuzuia vitisho vya kitaifa, kikanda na kimataifa.

Idara ya Usalama wa Taifa ya Ethiopia pia imekamata aina mbalimbali za madini yakiwemo kilo 44 ya dhahabu iliyokuwa ikijaribu kutoroshwa nje ya nchi.

TRT Afrika