Majeruhi wengi wahofiwa baada ya milipuko miwili mikubwa ya bomu kuutikisa mji wa kusini magharibi wa Somalia wa Bardhere katika eneo la Gedo Jumatano.
Milipuko hiyo ililenga kambi ya jeshi la taifa la Somalia na vikosi vya Ethiopia vinavyohudumu chini ya ujumbe wa wa Mpito wa Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS), kulingana na waziri wa mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi Adan Aw Hirsi.
"Askari wetu walizuia bomu la kujitengenezea la kulipua magari lakini kwa bahati mbaya la pili lililipuliwa," alisema katika taarifa fupi kwenye Twitter.
"Al Shabaab na (wale) waliowafadhili kufanya mashambulizi haya hawataweza kututisha," aliongeza.
Wakaazi wa Bardhere waliambia Shirika la Anadolu kwa njia ya simu kwamba milio ya risasi ilitokea baada ya milipuko hiyo.
Hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na shambulizi hilo, lakini kundi la kigaidi la Al Shabab lilidai kuhusika na mashambulizi ya hivi karibuni katika taifa hilo la Pembe ya Afrika.