Serikali ya Nigeria imesema hakuna kurudi nyuma katika uamuzi wake wa kusitisha ruzuku ya mafuta  Picha: Reuters

Na Charles Mgbolu

Serikali ya Nigeria imesema hakuna kurudi nyuma katika uamuzi wake wa kusitisha ruzuku ya mafuta ambayo ilifanya bei ya mafuta nchini humo kuwa ya chini zaidi duniani.

Ni uamuzi mchungu ambao tayari umekuwa na athari kwa maisha ya Wanigeria wa kawaida, na kupeleka bei za bidhaa na huduma kote nchini kupanda juu.

Katika hotuba yake ya kuapishwa Mei 29, rais mpya wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu alitangaza bila shaka kwamba kuongezeka kwa gharama ya ruzuku ya mafuta - zaidi ya dola milioni 800 kwa mwezi, kwenye akaunti ya Shirika la Kitaifa la Petroli la Nigeria na $10bn mwaka 2022 pekee - haikuwa swala endelevu.

Ruzuku kwa mafuta ilikuwa, na sababu nzuri, imekuwa sera maarufu sana, ikiibua manufaa ambayo yaliathiri moja kwa moja na kupunguza viwango vya maisha nchini.

Wakati bei ya mafuta ilikuwa chini huku kukiwa na mwelekeo wa mfumko wa bei duniani kote, bei za bidhaa na huduma nchini Nigeria ziliendelea kuweza kugharimiwa na mwananchi wa kawaida.

Tangazo la serikali kwamba itasimamisha malipo ya ruzuku, kwa hivyo, ilizua hofu.

Rais mpya wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu amesema ruzuku kwa mafuta itaondolewa Picha Reuters        

Raia wa Nigeria walikimbilia kwenye vituo vya mafuta ili kununua na kuweka mafuta kabla ya bei kupanda kwa kasi, na hii ilisababisha foleni ndefu kutokea mara moja katika vituo vya mafuta nchini kote.

Mbio hizo hazikufaulu, kwa kweli, kwani vituo vya mafuta vilipandisha bei mara baada ya hotuba ya rais.

Bei ya mafuta iliruka zaidi ya 200% kutoka $0.40 hadi $1.18.

Baadhi ya vituo vya mafuta viliacha kabisa kuuza mafuta.

Swala nyeti

Nigeria ni nchi yenye utajiri wa mafuta lakini inasafirisha nje bidhaa ghafi na kisha kuagiza bidhaa zilizosafishwa hasa kutoka Ulaya kwa sababu haina viwanda vinavyofanya kazi vizuri vya kusafisha.

Utaratibu huu unachangia pakubwa kwa bei ya juu ya mafuta na uhaba pia.

Uhaba ya mafuta Nigeria umeongeza gharama ya maisha ( Picha Reuters) 

Ruzuku hiyo hutolewa na serikali ili kupunguza bei inayolipwa na watumiaji wa nishati.

Kampuni ya mafuta inayomilikiwa na serikali, Nigerian National Petroleum Corporation Limited inasema bei mpya za pampu za mafuta zimerekebishwa ili kuakisi mienendo ya soko ya sasa.

Serikali ya Nigeria ilianzisha Ruzuku ya mafuta mwaka 1977 ili kupunguza athari za kupanda kwa bei ya mafuta duniani katika muongo huo, Hii ilikuwa chini ya utawala wa kijeshi wa Olusegun Obasanjo, ambao ulitangaza sheria ya kudhibiti bei ili kudhibiti gharama za bidhaa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mafuta.

Mnamo 2012, rais wa zamani Goodluck Jonathan alitangaza mipango ya kuiondoa, akitaja haja ya kuvutia wawekezaji zaidi kwenye sekta hiyo.

Hili lilizusha maandamano ya nchi nzima na shughuli za kiuchumi zilizokwama kwa wiki mbili.

Ingawa watu wengi sasa wanajua na kukubali kwamba malipo ya ruzuku yanalitia hasara taifa, kuondolewa kwake kunaathiri mapato ya wanigeria binafsi.

Uchungu wa ongezeko ya bei

"Si rahisi kwetu," Kenneth Umerie, mwenye umri wa miaka 29 ambaye anaishi Lagos, aliiambia TRT Afrika. "Hebu fikiria kulipa mara mbili ya nauli yako ya kila siku kwenye usafiri, kwani ninalazimika kufanya bila nyongeza ya kipato changu? Nitaishi vipi?"

Mkazi mwingine, Omolara Akerele, alisema athari za ruzuku ya mafuta kuondolewa zimeathiri mipango ya maisha ya kila siku ya familia.

"Mume wangu hawezi tena kurudi nyumbani baada ya kazi kwa sababu ya nauli ya usafiri kuongezeka mara mbili" analalamika.

"Akifanya hivyo hatutakuwa na chochote ifikapo mwisho wa mwezi. Sasa inabidi alale nyumbani kwa rafiki yake karibu na kazi na kurudi mara moja tu kwa wiki. Inawahuzunisha watoto ambao hawamwoni," Akerele anaongeza.

Jide Pratt, mtaalamu wa uchumi mjini Lagos, anasema hapakuwa na wakati mwafaka wa kuondoa ruzuku.

Kulikuwa na foleni ndefu katika vituo tofauti vya mafuta nchini Nigeria baada ya kutangazwa kuwa ruzuku itaondolewa ( Picha AA )

"Siku zote kutakuwa na athari kwa fedha zetu kwa sababu, kama Wanigeria, tumekuwa hatuishi katika uhalisia. Tumekuwa hatulipi thamani ya soko ya bidhaa hiyo." Anaamini kuwa watu wana uchungu "kwa sababu hakujawa na mawasiliano yoyote ya wazi ambayo yanasema hivi ndivyo ingefanywa na akiba inayotokana na kutolipwa kwa ruzuku".

Mawimbi kwa majirani

Nigeria haiko pekee, jirani yake Ghana pia ilitangaza mwezi Aprili kwamba ruzuku imeondolewa ili kuleta utulivu katika sekta yake ya chini.

Lakini huku Wanigeria wakiugulia chini ya uzito wa ghafla wa kifedha ambao wamelazimika kubeba, vyama vya wafanyikazi vimeongeza shinikizo kwa serikali kubadili uamuzi huu.

Mgomo wa kitaifa uliopangwa kufanywa na Bunge la Nigeria la Labour Congress ulisitishwa wakati wawakilishi wa serikali wakikimbia kutafuta mwafaka wa kati na makundi tofauti ya waandamanaji.

Ingawa wengine wanahisi shinikizo la kudumu linaweza kugeuza uamuzi huo kichwani mwake, mwanauchumi Pratt anasema kuwa Rais Tinubu hatabadilisha uamuzi wake,

"Ninaamini Tinubu anataka kusahihisha masimulizi kuhusu yeye mwenyewe kabla ya kuwa Rais kwa hivyo, asingesema asichomaanisha au mambo ambayo hawezi kutekeleza," anasema.

Kiwanda cha kusafisha mafuta cha kampuni ya Dangote kilivumbuliwa Mei 2023 ( Picha Reuters )

Pengine rais Tunubu ana hoja ya kuwathibitishia wakosoaji wanaotilia shaka uthabiti wake wa kuongoza nchi. Kuimarisha uamuzi huu na kuthibitisha manufaa yake kungekuwa mafanikio yaliyochongwa kwa jina lake

"Lakini kuna haja ya kuwa na suluhu - ikiwa wanasema kwamba mafuta yanapanda kwa kiasi fulani, basi kiasi hicho kinafaa kuingia kwenye mishahara. Tunahitaji kuweka kitu kama hicho mahali pake," Pratt anapendekeza.

Mnamo Mei 22, watunga sera na waendeshaji wa viwanda kutoka duniani kote walikusanyika Lagos kwa ajili ya kushuhudia kuanzishwa kwa kiwanda kikubwa zaidi cha kusafisha mafuta . Kiwanda hiki chenye uwezo wa kuchakata mapipa 650,000 kwa siku,

Kiwanda hiki kimejengwa na kampuni ya kundi la Dangote. Hii imeongeza matumaini ya usafishaji wa mafuta ya petroli wa ndani ya nchi lakini kiampuni bado hakijaanza kazi kikamilifu.

" Uwezo wetu wa kusafisha mafuta unavyoongezeka nchini Nigeria, ndivyo tutakavyokuwa kama muuzaji bidhaa nje bora na sio mnunuzi kutoka nje. Hii inamaanisha mapato zaidi, na ikiwa serikali ina nia ya kupunguza upotevu, basi nadhani tutaona mabadiliko ya kufurahisha kiuchumi," Pratt anasema.

TRT Afrika