Na Dayo Yussuf
''Hakuna kikubwa cha kusherehekewa,'' kuhusu afua ya deni ya Zambia asema Conrad Masabo, mhadhiri msaidizi wa sayansi ya siasa na utawala wa umma, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Habari zilitokea kwamba Zambia imepewa idhini ya kurudia upya mfumo wa kulipa madeni yake ya nje, maarufu kama 'Debt restructuring,' katika kikao cha viongozi wa dunia mjini Paris.
Lakini kwa mujibu wa mtaalamu na mwalimu wa Chuo Kikuu, Conrad Masabo, hili ni suluhisho la muda mfupi kwa tatizo kubwa.
''Kilichotokea Zambia, haijasamehewa deni, kwa sababu walikuwa wanatarajia kwamba China ambayo inawadai dola bilioni 4.1 moja ingekubali kuwasamehea sehemu ya deni,'' aliambia TRT Afrika. '' Walichokipata Zambia ni afua ya kuchelewesha kulipa deni kwa kupata kipindi cha neema cha miaka mitatu kisha kuchelewesha kulipa deni kwa muda wa miaka ishirini.''
Elewa afua ya madeni -'Debt restructuring'
Tatizo la madeni linapotokea, kuna uwezekano wa nchi ama taasisi kutangazwa kuwa imefilisika, kama ilivyotokea nchini Sri Lanka.
Kwa hiyo huu utaratibu wa Debt restructuring, ni kujaribu kuleta afua nchi isiweze kutangazwa kuwa imefilisika.
''Ni utaratibu wa nchi iliyoingia katika mgogoro wa madeni, ikishaona kuwa haiwezi kulipa, inatafuta namna ili isiingie kwenye kufilisika na itafute njia mbadala kuendelea kulipa madeni yake.'' anasema Conrad.
'Debt Restructuring' inahusisha mambo matatu:
- Majadiliano juu ya kuahirisha muda wa kulipa deni lililo iva.
- Uwezekano wa kupunguza riba inayotakiwa kulipwa
- Kusamehewa sehemu ya deni hilo
Zambia kwa sasa ina deni la zaidi ya dola bilioni 32.8. Kati ya hizo, dola bilioni 18.6 ni deni la nje. Hii ina maana kuwa Zambia tayari inaorodheshwa katika walio na deni kubwa kupita kaisi.
Kati ya deni la dola bilioni 18.6, kiasi walichokubaliwa kuahirisha kulipa ni dola bilioni sita ambayo watapewa muda wa neema wa miaka mitatu kisha kulipwa kwa miaka ishirini, pamoja na riba.
Kutokana na mzigo wa madeni haya, Zambia ilikuwa mashakani kwani shirika la fedha duniani IMF lilikuwa limeahirisha kuipatia nchi hiyo fedha zilizoahidiwa, ikiwemo za kufadhili miradi ya dharura kama vile dola bilioni 1.3 zilizotarajiwa kupata za kukabiliana na Uviko -19 za nchi mbali mbali.
Sasa IMF itaweza kutoa takriban dola milioni 188 kwa Zambia walizokuwa wamezuilia.
Pia msamaha huu utaiwezesha Zambia kwa muda w amiaka mitatu kutokuwa na mzigo wa kulipa madeni na riba zake, kwa hiyo wataweza kutumia fedha wanazopata kwa maendeleo ya ndani ya nchi.
Pia mpango huu unaleta kuaminika kwa ipa nchi hiyo uaminika wa ustahimilivu wa uchumi kwa kiwango fulani.
''Hii inaewezesha sasa kusimamia uchumi wao, hata ikij akukamilika muda wa miaka mitatu ya neema wataweza kurudi kulip amadeni yao kama kawaida.'' Anasema mchambuzi Masabo.
Zambia wako na wenzao katika zogo hili la deni
Ghana tayari imo katika kutishiwa kushindwa kulipa madeni yake. Tayari wapo katika mazungumzo na IMF kujaribu kutafuta njia za kujikwamua wakiwa na Ethipia. nchi nyingine zilizokokatika tishio la mdororo wa uchumi ni Niger, Zimbabwe na hata Kenya ambayo imetajwa kwa kiasi flani kuanza kulemewa na mzigo wa madeni ya nje, baada ya kupata ugumu wa kulipa mishahara ya wafanyakazi hivi karibuni.
''Usipolipa mishahara ina maana kutakuwa hakuna uzalishaji, na mzunguko wa fedha utakuwa haupo, kwa hiyo uchumi utadorora,'' anasema Conrad. 'Lakini ukilipa mishahara unakuwa huna uwezo wa kulipa deni la nje. Ndicho kilichowatokea Kenya.'' ameongeza.
Zambia iliingia kwenye mgogoro wa ulipaji mwaka 2020, wakati wa Uviko-19. Ikawa nchi ya kwanza Afrika kushindwa kulipa madeni yake ya nje, ndipo ikalazimika kuomba kubadilishiwa utaratibu wa kulipa deni lake.
Katika hili deni kuna hela inadaiwa na Uingereza, China, Afrika Kusini, Ufaransa, India na hata Israel. Lakini ni lazima wadeni wote wakubaliane juu ya namna deni hilo litabadilishiwa utaratibu wa kulipa. Tatizo ni kuwa nchi zote hizi wanachama wa G20, zilikuwa zinavutana kwa zaidi ya miaka miwili.
Funzo kwa wengine
''Huu utaratibu wa kukopa kwa uwiano wa pato la taifa ni utaratibu ambao hauna afya kwa uchumi. Hiyo ina maana kuwa kuna vitu hukuangalia.'' Anasema Mchambuzi Conrad.
Mataifa ya Afrika yametakiwa kujifunza kutoka kwa mgogoro wa kiuchumi uliokumba Zambia na mataifa mengine ili kuepuka kuyarudia makosa.
Wataalamu wanashauri kuwa njia bora zaidi ni kuangalia zaidi ndani ya nchi katika kutafuta hela ya kuendeleza shughuli za nchi kuliko kukopa nje.
''Kule Tanzania tunapenda kutumia msemo, denini himilivu, yaani pato la taifa linaweza kumudu ulipaji wa madeni lakini hii lazima iangalie vigezo vya mkopo.'' Anaongeza Conrad. ''Kwa mfano, Tanzania ina uhimilivu wa 14.1% ambapo kiwango cha mwisho ni 15% kwa hiyo tunaonekana tunao uwezo wa kulipa. lakini kukitokea changamoto yoyote, tunaweza kujikut atumetumbukia katika kushindwa kulipa.'' anaongeza.
Conrad anashauri kuwa mikopo inayochukuliwa pia lazima yawe na faida fulani kwa nchi.
''Serikali inapokopa sana kwa ajili ya miundombinu tujue kwamba miundombinu inachukua muda mrefu kurejesha hela. Ni tofauti na mikopo inayochukuliwa kwa ajili ya kuwekeza, inayorejesha hela katika mzunguko na kuimarisha uchumi.''
Pia Conrad amesema kuwa ni muhimu kujua sababu za kukopa. Ni lazima mataifa yaangalie iwapo ni lazima kukopa au kupunguza matumizi za serikali.
''Nadhani nchi zetu zilitakiwa zipunguze gharama za uendeshaji wa serikali badala ya kukimbilia kukopa zaidi. Hiyo ndio changamoto kubwa inayozisakama nchi za Afrika. ameambia TRT Afrika, mchambuzi Conrad Masabo.