Vimelea vya kirusi cha Marburg./Picha: Getty

Serikali ya Marekani imewaonya raia wake wanaopanga kusafiri kuelekea nchini Rwanda kutokana na ugonjwa wa kirusi cha Marburg.

Wikiendi iliyopita, taifa hilo lilitangaza kuwa ugonjwa wa Ebola ulikuwa umeua watu 12, wengi wakiwa ni wafanyakazi wa sekta ya afya, toka kulipuka kwa ugonjwa huo mwisho wa mwezi uliopita .

Onyo hilo la kiwango cha tatu, limetolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

Maambukizi yaliyothibitishwa

Bodi ya Maendeleo Rwanda imesema kuwa hatua hizo za kutokusafiri zimewekwa kuanzia siku ya Jumapili.

Kulingana na bodi hiyo, abiria wote wanapimwa hali joto za miili yao huku vituo vyenye vitakasa mikono vikiwekwa katika sehemu za kuondokea.

TRT Afrika