Kampuni ya usambazaji umeme ya Afrika Kusini, Eskom, inasema itasitishamgao wa umeme ulioleta utata leo, Juni 6, kutokana na mahitaji ya chini yaliyo tarajiwa na kuboreshwa kwa uwezo wa kuzalisha umeme.
Kampuni hiyo inasema mgao wa umeme utasitishwa kutoka 08:00 hadi 16:00 GMT.
Tangu mwaka 2007, Afŕika Kusini imepambana kusimamia mifumo yake ya kuzalisha umeme, huku mgao ukipitishwa kuwezesha maeneo mbalimbali ya nchi kupata umeme kwa angalau saa chache kila siku.
Lakini hali hiyo imesababisha kukatika kwa umeme kwa njia isiyokuwa ya kawaida, na maeneo mengi yameachwa bila umeme kwa masaa au hata siku.
Eskom inasema kusitishwa kwa mgao kumewezeshwa zaidi na Waafrika Kusini ambao walitii wito wa kutumia umeme kwa uangalifu na kwa ufanisi, ikiwa ni pamoja na kuzima kutoka 17:00 hadi 21:00 GMT.
Eskom ilieleza hili lilisaidia kupunguza shinikizo kwenye mfumo wa umeme na kuchangia katika hatua za chini za upunguzaji wa mgao.
Wakati majira ya baridi yakikaribia, Waafrika Kusini walikuwa na wasiwasi kwamba uondoaji wa mgao ungeathiri sana maisha yao na waliitaka serikali kuingilia kati.