Kikosi cha Somali kimekuwa kikipigana na wanamgambo wa Alshabab kwa zaidi ya miaka 16. /Picha: Wengine

Serikali ya Somalia ilisema wanajeshi wake watano walikufa katika vita, huku wakiwaua karibia wapiganaji 50 kutoka kundi la wanamgambo la Al-Shabaab siku ya Jumamosi, takriban kilomita 350 kaskazini mwa mji mkuu, Mogadishu.

Wanajeshi wa serikali na vikosi vinavywaunga mkono walipata taarifa za shambulio lililopangwa na Al-Shabaab huko Ceeldheer, katika eneo la Galgadud, na hivyo kuwavizia, na "kuwaangamiza", ilisema taarifa.

Kulingana na mamlaka, vikosi vyao viliwauwa takriban wanachama 47 wa kundi la wanamgambo huku wakiwapoteza wanajeshi watano katika vita hivyo. Walisema mashambulizi ya anga pia yalitekelezwa dhidi ya vikosi vya Al-Shabaab.

Al-Shabaab walidai kuhusika na shambulio la Ceeldheer.

'Mapigano makali'

Mkazi wa eneo hilo Mohamed Hussein aliiambia AFP kwa simu: "Kulikuwa na mapigano makali katika mji wa Ceeldheer asubuhi ya leo baada ya Al-Shabaab kushambulia mji huo kutoka pande kadhaa.

"Ilikuwa vigumu sana kusema ni nani alikuwa akitawala muda mfupi uliopita, lakini sasa tunaweza kuona kwamba vikosi vya serikali ya Somalia viko katika udhibiti kamili," aliongeza.

Mwanmaume mwingine wa eneo hilo, Hassan Gutale, alisema, "Kulikuwa na milipuko mikubwa isiyopungua sita na mapigano ambayo yalichukua saa kadhaa."

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, aliyechaguliwa Mei 2022, aliapa kuanzisha "vita kamili" dhidi ya kundi hilo la wanamgambo.

Vita dhidi ya Alshabab vinaendelea kwa muda mrefu

Al-Shabaab imekuwa ikiendesha uasi mbaya dhidi ya serikali kuu dhaifu huko Mogadishu kwa zaidi ya miaka 16.

Ingawa walifukuzwa nje ya mji mkuu na kikosi cha Umoja wa Afrika mwaka 2011, bado wana uwepo mkubwa katika maeneo ya vijijini nchini Somalia.

Wamekuwa wakifanya mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya wanasiasa, walinzi wa usalama na raia, hasa nchini Somalia lakini pia katika nchi jirani, ikiwa ni pamoja na Kenya.

Serikali hio inayokabiliwa na hali ngumu nchini Somalia imeungana na wapiganaji wa makabila dhidi ya waasi hao, na kufaulu kudhibiti tena maeneo mengi katikati mwa Somalia, katika operesheni inayoungwa mkono na ujumbe wa AU unaojulikana kama ATMIS pamoja na mashambulizi ya anga ya Marekani.

Lakini mashambulizi hayo yamekabiliwa na vikwazo, huku Al-Shabaab mapema mwaka huu wakidai kuwa imedhibiti maeneo mengi katikati mwa nchi.

TRT Afrika