'Trilateral mechanism' , yaani utaratibu wa utatu , inajumuisha Umoja wa Afrika, Umoja wa mataifa na IGAD   / Photo: AFP

Hali nchini Sudan iko katika hali ya sintofahamu baada ya ghasia nchini Sudan kuanza tarehe 15 Aprili 2023.

Mgogoro kati ya jeshi la Sudan na Kikosi cha Rapid Support Forces, RSF, unatatiza juhudi za nchi hiyo kuelekea katika uchaguzi uliotarajiwa mnamo 2024 kwa ajili ya kupata kiongozi wa kiraia.

'Trilateral mechanism' , yaani utaratibu wa makubaliano ya pande tatu , ikijumuisha Umoja wa Afrika, Mamlaka ya Kiserikali ya Maendeleo, IGAD na Umoja wa Mataifa. imekuwa katika mstari wa mbele wa kutafuta suluhisho ya kusitisha vita nchini Sudan.

Je, ni juhudi gani zimefanywa na utaratibu huu tangu vita vianze tarehe 15 Aprili?

  • Tarehe 16 Aprili- IGAD ilifanya mkutano wa mtandaoni wa dharura wa marais kuhusu Sudan. Ikaamua marais wa Kenya, Djibouti na Sudan Kusini kama wapatanishi
  • Tarehe 16 Aprili - Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika lilifanya mkutano wa dharura kuhusu ghasia nchini Sudan
  • Tarehe 19 Aprili - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutteres alizungumza na rais wa Kenya William Ruto kuhusu hali ya Sudan
  • Tarehe 20 Aprili - Umoja wa Afrika uliandaa kikao cha dharura cha mawaziri kufuatia kuongezeka kwa migogoro nchini Sudan. Ikaomba Makubaliano ya pande tatu kutekelezwa kwa mpango wa dharura wa kukomesha mzozo nchini Sudan, kufanywa na ushirikiano na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, wajumbe wa Baraza la Katibu wa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, IGAD, Saudi Arabia, Qatar na Falme za Kiarabu
  • Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alisema ataendelea kutumia "ofisi zake nzuri" kwa uratibu wa karibu na washirika wa UN ili kutafuta juhudi za usitishaji wa vita, kuondoa mvutano na kuanzisha mazungumzo ya kisiasa.
  • Tarehe 22 Aprili -utaratibu wa Makubaliano ya pande tatu unaelewa umuhimu wa kufikia usitishaji wa muda mrefu wa uhasama kwa ajili ya Wasudan wote na mustakabali wao.

TRT Afrika