Mahakama Uingereza yamfunga seneta wa Nigeria na mkewe kwa njama ya kujipatia viungo vya binadamu

Mahakama Uingereza yamfunga seneta wa Nigeria na mkewe kwa njama ya kujipatia viungo vya binadamu

Wanandoa hao walihukumiwa siku ya Ijumaa kwa kula njama ya kupanga safari ya mwanamume ili kuvuna figo yake.
#JRU63 : Wakati wa kusubiri kusikilizwa kesi ya seneta wa Nigeria ya unyanganyi wa viungo / Photo: AFP

Mwanasiasa wa Nigeria, mke wake na daktari wamefungwa na mahakama ya Uingereza kwa kumpeleka mfanyabiashara wa mtaani wa Lagos mjini London mwenye umri wa miaka 21 ili kumdhulumu figo yake.

Seneta Ike Ekweremadu na mkewe Beatrice walitaka mwanamume huyo awe mfadhili wa binti yao, Sonia, ambaye anaugua ugonjwa wa figo.

Mshukiwa wa tatu, Dkt Obinna Obeta, pia amefungwa kwa kumlenga mfadhili anayetarajiwa.

Watatu hao walipatikana na hatia mwezi Machi kwa kuvunja sheria za kisasa za utumwa.

Ekweremadu alihukumiwa kifungo cha miaka tisa na miezi minane jela, huku Beatrice akifungwa miaka minne na miezi sita. Dk Obeta alihukumiwa kifungo cha miaka 10.

Mwanaume huyo aliyedaiwa kuwa mfadhili aliwasilishwa mnamo Februari 2022 kwa uwongo kwenye kitengo binafsi cha figo huko London kama binamu yake Sonia katika jaribio la upandikizaji ambalo halikufanikiwa.

TRT Afrika