Mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo Kusini mwa jimbo la Kivu mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, imesababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi, na kuuwa angalau watu 40, hayo ni kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani.
Angalau watu 20 wamepatikana wamekufa katika mji mkuu wa Bukavu huku miili mengine 20 imepatikana katika kijiji kilichopo karibu na mji wa Burhinyi, taarifa za Jumatano, kutoka ofisi ya gavana zimesema.
Jitihada za uokozi zinaendelea, huku kukiwa na wasi wasi wa kuongezeka kwa idadi ya vifo.
Mwezi Mei, mwaka huu, takriban miili 438 ilipatikana katika maeneo ya Kalehe, Kusini mwa Kivu eneo lililopata athari kubwa ya mvua.
DRC, mara kwa mara inakabiliwa na majanga ya asili katika msimu wa mvua.
TRT World