Muda mfupi baada ya kuchukua madaraka, Waziri Mkuu Dbeibeh alizuru Abu Dhabi, na kufanya majadiliano na mwana wa mfalme  Mohammed bin Zayed. / Picha: AA   

Na Fuat Sefkatli

Kutoka kuwa mmoja wa wafadhili wakubwa wa shambulio lililofeli la jenerali Khalifa Haftar dhidi ya Tripoli mwaka 2019, hadi kuwa kiungo muhimu aliyebadilisha mwelekeo kabisa katika mzozo tata wa kiraia, nchi ya UAE imefanya mabadiliko ya nyuzi 180 nchini Libya.

Tangu uteuzi wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) chini ya Abdulhamid Dbeibeh mwezi Machi 2021, maswali kuhusu nafasi ya UAE nchini Libya yamejadiliwa mara kwa mara.

Ili kuelewa kwa kiasi gani UAE imegeuza mwelekeo wake wa kiitikadi, msingi wa maslahi, na tamaa ya kijiografia, tangu kuanzisha ushiriki wake mkubwa nchini Libya mwaka 2016, ni muhimu kutazama kwa kifupi yaliyotokea hivi karibuni.

Mara tu baada ya kushika madaraka, Waziri Mkuu Dbeibeh alitembelea Abu Dhabi, ambapo alifanya mazungumzo ya pande mbili na Mfalme Mohammed bin Zayed, akilenga jukumu ambalo UAE inaweza kuchukua katika mchakato wa kujenga upya Libya.

Aidha, mwezi Julai 2022, UAE iliweza kuleta usuluhishi ya makubaliano ya kugawanya madaraka kati ya Dbeibeh na jenerali Haftar , ikicheza dori kubwa katika kumteua Farhat Ben Gadara kama mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Kitaifa ya Libya (NOC).

Katika kipindi hicho, UAE pia iliondoa ufadhili kwa wapiganaji wa Kiafrika katika mashariki mwa Libya, ikionyesha kuvunjika kwa makubaliano kati ya Haftar na Kampuni Binafsi ya Kijeshi ya Wagner (PMC) na UAE.

Zaidi ya hayo, ripoti zilizochapishwa na taasisi inayohusishwa na serikali, “Emirates Policy Center (EPC)” katika mwaka wa 2022 na 2023, zikisisitiza unganishaji wa benki kuu, utekelezaji wa mchakato wa uchaguzi, na kusitisha mizozo ya kisiasa, zinaeleza zaidi mwelekeo uliobadilishwa wa UAE nchini Libya.

Vigezo vya mabadiliko ya kimkakati

Kwanza, mabadiliko kutoka kwa utawala wa Trump kwenda kwa urais wa Joe Biden nchini Marekani kulileta uhusiano mgumu kati ya nchi za Ghuba, ikiwa ni pamoja na UAE na Saudi Arabia.

Utawala wa Biden ulichukua msimamo mgumu dhidi ya tabia fulani za kikanda, jambo lilosababisha UAE kutafuta muungano mpya na washirika wa kikanda.

Wakati muhimu katika marekebisho haya ya kimkakati, ilikuwa ni saini ya Makubaliano ya Abraham mwezi Novemba 2020, ambayo ilirahisisha uhusiano na Israel na kuashiria upangaji upya mkubwa katika siasa za kikanda.

Hii ilikua baada ya kuanzishwa kwa mchakato wa kukaribiana na Uturuki, kulisababisha kupungua kwa kasi kwa msimamo wa UAE katika kesi ya Libya.

Upande muhimu wa marekebisho haya ulikuwa ni kusitishwa kwa msaada wa kifedha kwa Wagner PMC na wapiganaji wengine wa Sudan na Chad wanaofanya kazi Mashariki mwa Libya.

Uamuzi huu unaweza kutafsiriwa kama mbinu ya kuepuka migogoro yanayoweza kutokea na Uturuki, taifa lenye ushawishi mkubwa kisiasa, kiuchumi, na kijamii katika Magharibi mwa Libya.

Zaidi ya hayo, kuanzishwa kwa uhusiano imara na GNU kulisisitiza mabadiliko ya UAE kutoka msimamo wa mzozo hadi ule unaolenga ushirikiano ndani ya muktadha wa Libya.

Pili, nafasi ya kimkakati ya Libya kama kitovu kinachounganisha Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara na Pembe ya Afrika hadi Bahari ya Mediteranea inaipa UAE faida kubwa, ikiwezesha udhibiti wa njia za biashara na kuongeza ushawishi wa kijeshi.

Katika muktadha huu, Libya inawekwa kama sehemu muhimu ya matumaini ya UAE ya kuwa kama njia ya biashara kati ya China na mataifa ya Magharibi.

Ndani ya mfumo huu wa kijiopolitiki, sehemu ya mashariki mwa Libya, kwa kiasi kikubwa ipo chini ya udhibiti wa Haftar, inaipa UAE fursa isiyo na kifani wa kujitokeza kama nchi yenye nguvu katika eneo hilo.

Hii inachangiwa kuwa ni karibu na Bahari ya Mediteranea, ambayo inatoa mali muhimu za bandari, na umuhimu wake wa kimkakati wa kuingiliwa katika maeneo mbalimbali ya mzozo barani Afrika.

Hasa, mtandao wa vifaa wa kijeshi uliowekwa huko ni muhimu kwa Sudan na Chad, nchi ambazo UAE ina ushiriki moja kwa moja.

UAE imejitahidi kufanya thabiti hadhi yake kikanda kwa kutumia miundo ya kijeshi ya nchi za Magharibi (Marekani, Ufaransa, Uingereza) na mashirika ya kimataifa (UM, NATO) yaliyopo Libya.

Hali hii inaonekana kuipa UAE jukwaa la kuonyesha uwezo wake na rasilimali kwa washirika wa Magharibi. Walakini, upinzani unaongezeka dhidi ya kuzuia mafuta mashariki mwa Libya kulisababisha marekebisho ya ushirikiano wa UAE katika eneo hilo.

Mabadiliko haya yameathiriwa sana na jumuiya ya kimataifa, haswa Marekani na mataifa ya Ulaya, wanaoendeshwa na dharura ya kustawisha mgogoro wa nishati ulimwenguni.

Zaidi ya hayo, juhudi imara za kidiplomasia zilizojengwa na serikali ya Dbeibeh na nchi hizi na UN, pamoja na makubaliano ya kimkakati katika sekta za nishati na ujenzi na GNU, zimechochea UAE kuelekea mwelekeo wa mantiki zaidi.

Jambo la tatu linalopaswa kuzingatiwa ni mabadiliko yanayoonekana katika msimamo wa UAE dhidi ya mapinduzi wakati wa awamu za mwanzo za mapinduzi ya Libya. Katika hatua za mwanzo za mapinduzi, baadhi walidokeza kuwa UAE iliona shughuli za kundi la “Muslim Brotherhood” nchini Libya kama tishio linaloweze kutishia kuendelea kwa utawala wake.

Mwelekeo wa mchakato wa kidemokrasia na kuingizwa kwa mfumo wa Kiislamu uliokuwa wa wastani, vilionekana na UAE kama viashiria vya kuanzisha harakati tofauti za kidemokrasia za Kiarabu.

Hisia hii ilisababisha UAE kumuunga mkono Haftar, ambaye alizindua kampeni dhidi ya vikundi vya kidini kwa sura ya 'sekula'. Walakini, mabadiliko katika muktadha wa kikanda na kimataifa, pamoja na sera za Haftar ambazo zilidhoofisha utulivu, zilijitokeza kama vyanzo vya wasiwasi kwa uongozi wa Abu Dhabi.

Hivyo basi, kujiondoa kwa Haftar hatua kwa hatua kutoka kwa udhibiti wa Misri na UAE kulipelekea mataifa haya kutafakari juu ya muungano mbadala.

Kupima Ushawishi: Mkakati katika Mabadiliko ya Usalama

Katika mabadiliko ya mazingira ya usalama ya Libya, njia ya UAE imekuwa wazi, na mwakilishi wake wa UN, Mohamed Abushabab, akizungumza wakati wa vikao vya Baraza la Usalama mwezi Aprili na Desemba 2023.

Abushabab aliipongeza juhudi za Abdoulaye Bathily, mwana diplomasia kutoka Senegal chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya (UNSMIL), katika kuandaa mikutano ya Kamati ya Kijeshi ya Pamoja ya 5+5, inayojumuisha maafisa wa kijeshi kutoka Tripoli na Benghazi.

Zaidi ya hayo, Abushabab alisisitiza haja kubwa ya kuanzisha mipango ya kudhibiti, na kupunguza uhamasihaji, na program za kuunganisha jamii ili kuunganisha vikundi vya kijeshi katika mikoa ya mashariki na magharibi ya Libya.

Mtazamo huu unathibitisha mabadiliko kutoka kwa msimamo wa awali wa UAE, ukiashiria mwelekeo wa kisasa wa kukuza muktadha wa kijeshi wa kuleta ustawi ndani ya Libya.

Hata hivyo, inaweza kuwa ni jambo la kufikirika kudai kwamba UAE inaweza kuchukua jukumu muhimu katika kurahisisha kupokonya kwa silaha na kuunganisha jamii haswa katika upande wa mashariki.

Hatimaye, taarifa ya mwezi Disemba 2023 zilipendekeza kuondolewa kwa vikosi vyote vya kijeshi vya kigeni na wapiganaji wa kulipwa kutoka Libya.

Msimamo huu unapendekeza kwamba, angalau kwa muda mfupi hadi wa kati, UAE haiwezi kurudi kutumia mikakati mbadala kwa maslahi yake.

Ni muhimu kutambua umuhimu wa mkakati wa uwepo wa kijeshi wa Uturuki katika eneo hilo, ambao ni muhimu kwa kuhakikisha utulivu na amani na hutumika kama kizuizi dhidi ya wachochezi.

Katika hali ya sasa ya kuboresha uhusiano kati ya Uturuki na Misri, kuna matarajio ya UAE kupunguza siasa zake na kufuata njia za ushirikiano wa kisiasa na kijeshi, na Uturuki, hasa linapohusiana na muktadha wa Libya.

Mwandishi, Fuat Emir Sefkatli, ni Mtafiti wa Maswla ya Kaskazini mwa Afrika katika Center for Middle Eastern Studies (ORSAM) huko Ankara.

TRT Afrika