Maafisa 531 wa Kikosi Maalum cha Operesheni nchini Rwanda wamehitimu na kujiunga na Jeshi la Rwanda (RDF)/ Picha    RDF

Maafisa 531 wa Kikosi cha Operesheni maalum nchini Rwanda wamehitimu na kujiunga na Jeshi la Rwanda (RDF).

Hii ni baada ya kumaliza mafunzo ya ya kivita ya miezi 11 katika Kituo cha Mafunzo cha Kijeshi cha Nasho, Wilaya ya Kirehe.

Kundi la waliohitimu linajumuisha Maafisa 46 na vyeo vingine 485.

"Lazima muimarishe ari na ujuzi mulioonyesha wakati wa masomo wakati wowote munapoitwa kutetea uhuru wa nchi yetu. Muwe tayari kutekeleza misheni yoyote kama wafanyikazi wa Kikosi Maalum cha Operesheni, "Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Rwanda Jenerali MK Mubarakh aliambia maafisa hao.

Katika kipindi cha miezi 11 ya Mafunzo ya Operesheni Maalum, maafisa hao walipewa mafunzo ya hali ya juu kwa ajili ya operesheni maalum, ikiwa ni pamoja na utumiaji wa silaha nzito na silaha ndogo pamoja na vita vya uso kwa uso.

Maafisa hao pia wamefunzwa mbinu za kuvuka mto na maeneo ya maji wakati wa vita, usomaji wa ramani ya kijeshi, upelelezi, ufundi wakiwa vitani, mbinu za kupanda milima na wanavyotakiwa kufanya wakiwa pamoja na kutowa huduma ya kwanza.

Ujuzi huu unalenga kuandaa vikosi vya RDF kutetea mipaka yao na kulinda uhuru wa taifa la Rwanda.

TRT Afrika