Hadi sasa, mamilioni ya raia wa nchi hiyo wanaendelea kuteseka huku Sudan ikiendelea kukabiliana na vita kati ya jeshi la nchi hiyo dhidi ya wanamgambo wa RSF. /Picha: NRC

Na

Abdulwasiu Hassan

Janga la kibinadamu nchini Sudan linaendelea kutokea kimyakimya licha ya Shirika la Norwegian Refugee Council (NRC) “janga kuu zaidi ulimwenguni ".

Hadi sasa, mamilioni ya raia wa nchi hiyo wanaendelea kuteseka huku Sudan ikiendelea kukabiliana na vita kati ya jeshi la nchi hiyo dhidi ya wanamgambo wa RSF.

Takwimu zinaonesha kuwa zaidi ya watu milioni 10 wamegeuka kuwa wakimbizi, huku idaidi ya vifo ikifikia 20,000.

"Inashangaza kuona tunashindwa kuwasadia mamilioni ya watu wanaokabiliwa na njaa," anaiambia TRT Afrika.

Yatazamwa kwa kina

Hadi kufikia sasa, jumuiya ya kimataifa imeshindwa kupitisha azimio la kumaliza mapigano nchini Sudan, achilia mbali kushinikiza kusitishwa kwa vita hivyo.

Hasina, ambaye kiasili anatokea Ethiopia, aliimbia Khartoum akiwa na watoto wake watatu mara baada ya kuanza kwa machafuko./Picha:/NRC

Hali hiyo inakuja huku vita nchini Sudan vikiendelea kusambaa katika majimbo 18.

"Sudan inakabiliana na hali mbaya kwa sasa. Watu wapatao milioni 11 wamekosa makazi nchini mwao wenyewe huku wengine milioni tatu wakiishi kama wakimbizi kwenye nchi jirani," anasema Egeland.

Hali hiyo inaliweka taifa hilo pabaya kwa sasa.

"Tunalazimika kukabiliana na janga kubwa zaidi la njaa ulimwenguni kwa sasa. Watu wapatao milioni 20 wanahitaji msaada wa kibinadamu. Msaada ni mdogo japo vikwazo vya kufikisha misaada hiyo ni vingi,” anasema Katibu Mkuu huyo wa NRC.

Makundi ya watu yameendelea kuukimbia mji wa Darfur kuepuka vurugu na njaa.

Hali hiyo inakuwa huku vita nchini Sudan vikiendelea kusambaa katika majimbo 18./Picha: NRC

"Tulichokiona Darfur ni makundi ya watu yakiendelea kuhama kila siku, hususani katika eneo la El Fasher kaskazini mwa Darfur kutokana na mapigano na mahitaji ya chakula na kukosekana kwa misaada huko Geneina, ambao ni mji mkuu wa Magharibi mwa Darfur," Egeland anaimbia TRT Afrika.

"Nimejionea maeneo mengi yakiwa yameharibika, yamevamiwa, ikiwemo ofisi yetu."

Licha ya mapigano hayo, mashirika ya kutoa misaada bado hayajakata tamaa.

Kulingana na Egeland, Shirika la NRC limeendela kutoa misaada kusini, Mashariki na kaskazini mwa Sudan.

Misaada hiyo ni pamoja na unga wa ngano wenye ruzuku kutoka Uturuki.

Wito wa msaada

NRC inalenga kuongeza misaada yake.

Kulingana na Egeland, Shirika la NRC limeendela kutoa misaada kusini, Mashariki na kaskazini mwa Sudan./Picha:NRC

Changamoto kubwa ya kukabiliana na njaa inaweza kuwa ngumu zaidi isipokuwa msaada zaidi uwasili, pamoja na mpango wa kimataifa wa kushinikiza pande zinazopigana kuruhusu wafanyakazi wa misaada kuwafikia raia wanaoteseka.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

TRT Afrika