Juhudi za Nigeria za kufufua huduma yake ya afya iliyolemewa, kupitia mchanganyiko wa hatua za kuzuia kuondoka kwa wingi kwa wataalamu wa Afrika na kuwarudisha nyumbani walio nje zimetoa matokeo mbali mbali hadi sasa.
Dk Kamar Adeleke, daktari bingwa wa upasuaji wa moyo ambaye aliacha kazi yake iliyoshamiri nchini Marekani na kurejea Nigeria alikozaliwa, ni miongoni mwa wachache waliojibu kile anachoeleza kuwa wito wa dhamiri yake.
"Kama singekuja Nigeria na badal ayake niende nchi za ng'ambo, Mungu angeniuliza imekuwaje sikuisaidia nchi yangu wakati inanihitaji?" anaambia TRT Afrika juu uamuzi wake wa kurejea kwa asili yake.
Dk Adeleke anakumbuka kusikia wajibu wa kurejea Nigeria, baada ya ziara ya hamasisho ya matibabu nchini humo, aligundua kuwa ugonjwa wa moyo ulikuwa mojawapo ya sababu kuu za vifo kati ya Wanigeria wa tabaka la kati.
Sio daktari pekee wa Nigeria aliyeamua kurudi ''kulikozikwa kitovu chake".
Idadi kubwa ya wataalam wa matibabu kama Adeleke wamechukua wito mgumu wa kurejea nyumbani na kuacha ustawi na mafanikio ya kitaaluma katika nchi za kigeni.
Hadithi za waliorejea, hata hivyo, zinazama katika mjadala juu ya kuendelea kuhama kwa wahudumu wa afya kutoka nchi yenye watu wengi zaidi barani Afrika na bara zima kwa ujumla.
Kinyume na ubinadamu
Kuhama kwa wataalam wa matibabu kutoka Afrika, au nchi yoyote katika ulimwengu unaoendelea kwa suala hilo, sio jambo geni.
Lakini mataifa kadhaa barani kote sasa yanazidi kuwa na wasiwasi kuhusu hali hiyo.
Kuanzia Ghana huko Afrika Magharibi hadi Zimbabwe Kusini mwa Afrika na Kenya katika Afrika Mashariki, viongozi wameachwa wakiumiza vichwa vyao kwa kukata tamaa jinsi ya kukabiliana na shida ya ubongo
Mwezi Aprili, Makamu wa Rais wa Zimbabwe, Constantino Chiwenga, alinukuliwa na vyombo vya habari akisema nchi yake inapanga kuharamisha uajiri wa madaktari wake katika nchi nyingine.
Chiwenga, ambaye pia ni waziri wa afya wa Zimbabwe, alisema uajiri wa aina hiyo - haswa na mataifa yaliyoendelea ya Magharibi - ulikuwa mbaya kwa nchi yake ambayo imeshuhudia kuhama kwa wataalam wa afya katika miaka ya hivi karibuni.
"Iwapo mtu ataajiri kimakusudi na kuifanya nchi iteseke, huo ni uhalifu dhidi ya ubinadamu. Watu wanakufa hospitalini kwa sababu hakuna wauguzi na madaktari. Hilo lazima lichukuliwe kwa uzito," Chiwenga aliripotiwa akisema.
Huko Nigeria, kampuni ya wakala wa kuajiri wataalamu ilikuwa Abuja mwaka jana kutafuta wataalam wa matibabu wa Nigeria kwa kazi za Uingereza.
Taswira ya madaktari wengi wakipanga foleni kwa ajili ya mahojiano ya kazi ilikuwa ya kuogofya kwani nchi hiyo ya Afrika Magharibi ilijaribu kudhibiti kile kinachojulikana kama japa, au harakati za ghafla kuelekea maisha bora nje ya nchi.
Kurudi nyumbani
Ingawa Uingereza baadaye ilisitisha uajiri wa madaktari kutoka nchi zinazoendelea kama Nigeria, hakuna dalili bado ya kusitishwa kwa msafara huo. Mswada unaotaka kuzuia kwa uhamaji wa madaktari umewasilishwa katika bunge la Nigeria.
Huku kukiwa na umaarufu unaotolewa kwa hadithi za madaktari kuondoka Nigeria, baadhi wanarejea tena kuchukua jukumu katika sekta ya afya ya nchi hiyo, wakisema hali sio shwari nje kama inavyodaiwa.
Lakini pia wanalalamikia vifaa duni nyumbani. Ukosefu wa vifaa vya kutosha inaweza kuwa moja ya sababu kwa nini matajiri na wanasiasa wakuu mara kwa mara husafiri nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.
Baadhi ya wataalamu wa matibabu wanaorudi nyumbani huchangia kwa njia ya kutoa mafunzo kwa kizazi kijacho cha madaktari na kubadilishana uzoefu waliopata nje ya nchi.
Hakuna njia ya mkato
Dk Abubakar Sa’idu, ambaye kwa sasa anafanya kazi katika Hospitali ya kitaifa ya Kufundisha ya Gombe katika sehemu ya kaskazini-mashariki mwa Nigeria, ni mmoja wa wale waliorejea nyumbani wakiwa na utaalam unaohitajika kuimarisha huduma za afya nchini humo.
Dk Sa’idu alikuwa anafanya kazi katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha King Khalid huko Riyadh, Saudi Arabia, kwa miaka mitano kabla ya kurejea Nigeria ili aweze kuwalea watoto wake "nyumbani na kuwa na wazazi wake".
"Ndiyo, kazi ilikuwa ngumu sana, lakini mna vifaa bora zaidi; kwa hivyo, inafurahisha sana," anaiambia TRT Afrika kuhusu uzoefu wake wa kufanya kazi nchini Saudi Arabia.
Mwishoni mwa mwaka jana, rais wa Chama cha Madaktari cha Nigeria, Uche Rowland, alisema zaidi ya madaktari 5,600 wa Nigeria walihamia Uingereza katika kipindi cha miaka minane iliyopita.
Akiwa amefanya kazi nchini Nigeria na nje ya nchi, Dk Sa’idu anaamini hakuna njia ya mkato katika kujaza pengo lililoachwa na wataalamu wa matibabu wanaoondoka Nigeria.
Kulingana na chama hicho, Nigeria ina takriban madaktari 24,000 waliosajiliwa nchini humo, na ingehitaji zaidi ya 360,000 ili kuweza kufikia usawa wa idadi ya madaktari na wagonjwa unaopendekezwa na WHO.