Wakristu katika sehemu tofauti duniani wanasherehekea krismasi 25 Disemba 2024  / Picha: Reuters / Photo: AFP

Msimu wa krismasi umefika.

Ni wakati watu kufurahia na kujumuika pamoja katika milo mitamu iliyoandaliwa. Huku wengine, wakienda vijijini wanaposubiriwa kwa hamu na ndugu, jamaa na marafiki ambao hawajawaona kwa muda mrefu.

Hata hivyo, msimu huu unaweza usiwe na furaha kwa wote. Msingi wa Krismasi ni Jerusalem ambapo katika mji wa Bethlehemu Yesu alizaliwa.

Siku ya Krismasi huko Bethlehemu, katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa/ picha: AFP

Lakini katika eneo hili mashambulizi ya Israeli dhidi ya Gaza yamesababisha maelfu kuyahama makazi yao na maelfu wengine kupoteza maisha.

Barani Afrika, kuna watu ambao pia hawataweza kuwa na Krismasi njema ikiwemo wale kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambapo vikundi vyenye silaha, na maafa mengine yamepelekea zaidi ya watu milioni 6.4 kuhama makwao.

Maelefu wameuawa kutokana na changamoto hizi. Pia milipuko wa magonjwa kama vile Mpox, Marburg na sasa ugonjwa usiotambulika ambao tayari umesababisha vifo vya watu kadhaa.

Padre akipita kati ya waumini wakati wa Misa ya Krismasi katika Kanisa Katoliki la Santa Maria Draperis katika wilaya ya Beyoglu huko Istanbul, Desemba 24, 2024, huku akibeba kiashirio cha kuzaliwa kwa Yesu./Picha AFP 

Nchini Sudan hakuna amani tangu Aprili 2023 huku jeshi la serikali ya Sudan likienedelea kupigana na kikundi cha Rapid Support Forces.

Mabadiliko ya tabia nchi nayo yamechukua nafasi yake ya kuleta huzuni na mfadhaiko katika jamii.

Goam kaskazini mwa DRC amabapo hakuna usalama kwas sababu ya vikundi vya silaha, hafla ya maonyesho yalifanyiak kuwapa nafasi raia wa eneo hilo la DRC kuonyesha ufanisi wao kwa kuunda nguo  (Picha / Jospin Mwisha / AFP)

Athari za Kimbunga Chido kilichopiga visiwa vya Mayotte, Madagascar na maeneo ya Msumbiji na Malawi bado inaonekana katika kusababisha vifo na kuleta uharibifu wa miundombinu. Yote haya, yamejiri katika mwezi huu wa Disemba.

Mbali na athari za Kimbunga, Krismasi nchini Msumbiji pia haitakuwa ya kawaida baada ya kuzuka kwa vurugu za baada ya uchaguzi hasa baada ya mahakama kumtangaza mgombea wa chama tawala Frelimo kuwa mshindi.

Na katika nchi ambazo zimesalimika na majanga asili, changamoto kubwa ni hali ngumu ya uchumi. Kama vile wanavyosema nyumbani, “hakuna pesa.”

Watu wanalalamika kupanda kwa bei za bidhaa huku wengine wakishindwa kugharamia shamra shamra za sikukuu ikiwemo watoto kuvaa vizuri, na kuandaa mlo maalumu kwa ajili ya sherehe.

TRT Afrika