Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Kenya ‘Harambee Stars’ Engin Firat, amejiuzulu nafasi yake.
Kulingana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Kenya (FKF) Hussein Mohammed, mchakato wa kumtafuta mbadala wake utaanza mara moja huku pia suala la kushugulikia madai ya mshahara wa kocha huyo raia wa Uturuki yakifanyiwa kazi.
Chini ya uongozi wa Firat, Harambee Stars ilishindwa kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), huku pia ikishindwa kushiriki michuano ya CHAN 2024.
Kenya ilitolewa kwenye hatua ya kufuzu AFCON 2025, mara baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi J, nyuma ya Cameroon na Zimbabwe.
Inadaiwa kuwa, kocha huyo akilipwa Dola za Kimarekani 15,473.
TRT Afrika