Paul Kalambay Otepe alicheza tim ya taifa ya Zaire iliyoshinda Kombe la taifa bingwa Afrika 1974 / Picha : wengine 

Shirikisho la soka Afrika CAF limetuma rambi rambi kwa familia jamaa na marafiki wa mlinda goli wa zamani wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo Paul Kalambay aliyefariki dunia Jumanne.

Rais wa CAF Dkt Patrice Motsepe amemsifia marehemu Kamlambay kama mmoja wa waasisi wa soka ya DRC na Afrika kwa jumla.

Paul Kalambay alifariki mjini Kinshasa Jumanne 12 Novemba 2024 ikiwa sambamba na siku yake ya kuzaliwa 12 Novemba 1948 akiwa na umri wa miaka 76.

Kalambay alikuwa sehemu ya Timu ya Taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iliyoshinda Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka wa 1974.

Timu hiyo pia ilikuwa ya kwanza kusini mwa jangwa la sahara kuwahi kufuzu fainali ya kombe la dunia mwaka 1974.

Kalambay alizaliwa Paul Mohammed Kalambay Otepa mnamo 12 Novemba 1948 nchini Congo wakati huo Zaire.

Amechezea timu ya taifa na klabu ya TP Mazembe kama kipa katika taaluma yake.

Atazikwa Jumatano 13 Novemba kulingana na utaratibu wa dini ya kiislamu.

TRT Afrika