‘Mti huu umeyaona yote yaliyotokea humu nchini.’ anasema Omar Farouk, mkaazi wa Freetown anayeomboleza kuanguka kwa mti mkongwe wa Mpamba uliokuwa katikati mwa jiji la Freetown.
Braka ya mvua iliyokuwa ikinyesha, iligeuka kuwa karaha kwao baada ya mafuriko ya mvua kusababisha kuanguka kwa mti huo.
Ukiwa umepasuka katikati, sehemu ya juu ya mti ulitapakaa katika barabara inayoelekea jengo la Mahakama Kuu, na kufunga njia.
Mpambo huo mkongwe pia umesimama katika njia panda ya barabara ya Siaka Stevens, iliyotolewa jina la rais wa zamani wa nchi aliyekuwa madarakani kwa miaka 17.
Katika taarifa yake ya kuaga, Rais Stevens aliutaja mpamba huo, pamoja na popo na tai waliokuwa wakiisha ndani yake.
‘‘Inahuzunisha sana kuuona mti ukiwa hivi,’’ anasema Omar. ‘Nimekulia kuuchezea mti huu, nimekuwa na mikutano chini yake, nimeketi hapa kupiga gumzo na marafiki, yaani nimekua na mtu huu.’’ aliongeza.
Wengi walioutambua mti huu wanasema kuwa wanahisi kama vile wautaje kama binadamu. Wanasema mti huo ulikuwa kama familia.
Hassan, aliyekulia mjini Freetown anasema alishtushwa na habari za kuanguka kwa mti huo. ‘‘Umekua kama mmoja wa familia. Nahisi kama vile nimempoteza mmoja wa jamaa zangu.’’
Omar ambaye alikwenda kujionea mwenyewe mabaki ya mti huo anasema, ''tulikuwa tukiwaelekeza wageni kwa kutumia mti huo. Ukifika katika mti, pinda kushoto au kulia..ilikuwa njia rahisi zaidi ya kuwapa watu maelekezo.''
Mbali na kutoa muelekezo, mti huo ulikuwa na uhusiano mkubwa zaidi na wenyeji. wanahistoria wanasema kuwa takriban watumwa walio achiliwa huru wapatao 4000 walitua katika nchi hiyo na moja kwa moja wakaja kwa mpamba huo na kufanya misa ya kurudisha shukrani kwa Mungu.
Utamaduni na imani
Kuna msemo maarufu wa lugha ya Krio nchini Sierra Leone, '‘Big breeze blow, Cotton tree foddom’ yaani kumaanisha, ‘‘ Mvua kubwa imenyesha na upepo mkali kuvuma, mpamba umeanguka.'' Wengi wanautumia msemo huu kumaanisha kuwa jambo baya limetokea.
Hassan anasema kuwa wazazi wake waliamini hilo. ‘'sijui kama kuna ukweli wowote hapo lakoini ni kiitu kilichozemwa na wengi mtaani kwetu. na bado mimi n arafiki zangi bado tunasema hivyo.’’
Rambi rambi zinaendelea kutolewa
Mti wa mpamba, maarufu zaidi nchiin Sierra Leone, limepewa majina mengi. kabila la Themne, waliuita Poolon, jamii ya Kono linauita Bandaa nao wa Mandingo wanauita Famba.
kwa jina lolote lile, ni nembo inayotambulika na taifa nzima. Rais Julius Maada Bio alikuwa miongoni wa watu wa kwanza kutoa rambi rambi kwa taifa. '' Tutaweka kitu kingine mahali hapo kitakachoweza kuwaunganisha wanachi wetu, na kuendeleza historia ya mpamba huo. Tutawashirikisha kila.”
Omar Farouk Sesay, ni mtunzi wa mashairi aliyeandika wimbo kwa heshima ya mti huo. anatumai kuwa maneno yake yatasaidia wananchi wa Siera Leone kuukumbuka mti wao.
Katika shairi lake, 'Mpamba wetu umetuacha,'' ameusifu mtu huo huku akiufanaisha na jengo la Eifle Tower ya Ufaransa, au sanamu la Liberty la New York.