Kikosi cha Harambee Stars kilichotwaa ubingwa katika mashindano ya mataifa manne, yaliyomalizika Machi 26, nchini Malawi./Picha: Malawi Football Federation

Mabao matatu kutoka kwa mshambuliaji nyota wa Al-Duhail ya Qatar, Michael Olunga yalitosha kuipa Harambee Stars ya Kenya ubingwa wa mashindano ya mataifa manne dhidi ya Mashujaa wa Zimbabwe, katika mchezo wa Fainali uliofanyika katika uwanja wa Bingu, mjini Lilongwe nchini Malawi.

Michuano hiyo ilikuwa na sehemu ya maandalizi ya 'Harambee Stars' kwa ajili ya michezo ya kundi 'F' dhidi ya Burundi na Ivory Coast, itakayofanyika Juni 3 na 10, mwaka huu.

Zimbabwe ndio ilikuwa ya kwanza kutangulia kushinda mchezo huo kufuatia bao la kujifunga la mlinzi wa 'Harambee Stars' Joseph Okumu, katika dakika ya nne ya mchezo.

Nahodha wa 'Harambee Stars' na nyota wa mchezo huo, Michael Olunga akifurahia ushindi wa timu yake ya taifa./Picha: Malawi Football Federation

Iliwachakua 'Harambee Stars' dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza kusawazisha bao hilo, kupitia kwa nahodha wao Michael Olunga, ambaye pia alikuwa anasheherekea siku yake ya kuzaliwa katika mchezo huo.

Goli hilo lilifuatia kazi nzuri iliyofanywa na Ayub Masika.

Karamu ya magoli kwa 'Harambee Stars,' iliendelea tena katika dakika ya 65, kupitia kwa Olunga tena, akimalizia mpira uliotemwa na golikipa wa timu ya taifa ya Zimbabwe, Bernard Donovan baada ya shuti kali la Rooney Onyango.

Michuano hiyo ilikuwa na sehemu ya maandalizi ya 'Harambee Stars' kwa ajili ya michezo wa kundi 'F' dhidi ya Burundi na Ivory Coast, itakayofanyika Juni 3 na 10, mwaka huu. /Picha: Malawi Football Federation

Dakika tatu kabla ya mchezo kumalizika, Olunga aliifungia Kenya bao la tatu, katika mchezo ambao timu zote zilimaliza zikiwa na wachezaji kumi kila upande, baada ya kuzawadiwa kadi nyekundu.

TRT Afrika