Serikali ya Kenya imetoa maagizo mapya katika uuzaji wa mitungi ya gesi.
Kanuni hizi zinakuja takriban mwaka mmoja baada ya mlipuko mbaya wa gesi uliotokea Februari 2024 na kusababisha vifo vya watu sita na kujeruhi zaidi ya 200.
Chini ya kanuni mpya wahusika wa uuzaji wa gesi ya matumizi ya nyumbani sharti wapate leseni kwa kila shughuli, ikiwemo uagizaji, usafirishaji, uhifadhi, ujazaji, usambazaji na uuzaji rejareja.
Kipengele kimoja ambacho wauzaji gesi wamelalamikia ni maagizo ya kununua au kujaza mitungi ya gesi ambayo inafaa kufanyika kati ya saa kumi na mbili asubuhi na saa kumi na mbili jioni.
Kando na muda huo, ujazaji wa gesi utafayika kama ulivyoidhinishwa na Kando na muda huo ujazaji gesi utafayika kama ulivyoidhinishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli (EPRA).
Zaidi ya hayo, wahusika wa sekta hiyo wameibua wasiwasi juu ya kuongezeka kwa idadi ya wamiliki wa mitungi ya gesi kutoka 30,000 hadi 70,000 chini ya kanuni zilizopendekezwa wakibainisha kuwa itakatisha tamaa biashara.
Kanuni hizo pia zinahitaji wanunuzi wa gesi kulipa fedha kiasi wakati wa kupata mitungi ya LPG, na pesa hii lazima irejeshwe baada ya mtu kurejesha mtungi wa gesi. Kiwango hiki cha malipo ya awali kitawekwa na serikali.
Vile vile, vituo vya mafuta zimeambiwa ni lazima vizingatie saa za kazi zilizobainishwa ili kupunguza hatari, kwa ratiba zilizoamuliwa na miongozo ya ndani ya EPRA.