Rais wa Rwanda Paul Kagame anasema kutimiza mchakato wa nchi za Afrika kufanya biashara pamoja zaidi ni muhimu  / Picha: Reuters

Rais wa Rwanda Paul Kagame anasema faida ya eneo huru la biashara la bara la Afrika ni zaidi ya changamoto zinazokabiliwa katika utekelezaji wake.

"Kuna matatizo mengi kwa mfano watu ambao wanapotea katika kutafsiri maswala yanayohusiana na nchi zetu kufanya biashara zaidi barani, baadhi ya mambo ambayo wanafikiri ni muhimu kwao ni tafsiri potofu ya baadhi ya mambo kuhusu biashara hii, " alisema Jumanne katika mahojiano yake na waandhishi wa habari.

Nchi 46 zimeridhia mkataba wa biashara ya kibara ambayo una nia ya kuinua biashara kati ya nchi za Afrika.

Nia ya eneo huru la biashara Afrika, AfCFTA, ni kuunda soko moja la bara lenye wakazi wapatao bilioni 1.3 na pato la taifa la takriban dola za Marekani trilioni 3.4.

Utimizaji wake bado unachelewa kwa sababu kuna nchi ambazo zinahofia kuwa nchi zenye uchumi kubwa zitanufaika zaidi.

Pia kuna vikwazo kadhaa kati ya nchi za Afrika kama ushuru na visa kuhitajika kusafiri kwenda nchi nyingine. Kuna nchi zingine zinahofia kufungua mipaka kwa sababu ya biashara huru, huenda kukaongeza changamoto za kiusalama.

"Wakati fulani watu wanasema usiguse hii inahusiana na uhuru lakini ikiwa hautafanya hivyo, uhuru unabaki kuwa jina tu, uungwana unapaswa kujumuisha uhuru wa watu kufanya kazi ndani na katika nchi zote," Kagame ameongezea.

Ikitimizwa kikamilifu, Umoja wa Afrika inasema mfumo huu wa biashara utainua mapato ya Afrika ya kindani kwa dola bilioni 450.

TRT Afrika