Jinsi mashujaa wa Yola wanavyo pambana na magonjwa na hatari zilizojificha

Jinsi mashujaa wa Yola wanavyo pambana na magonjwa na hatari zilizojificha

Ni wanafanya kazi katika hospitali ya jamii kwenye jiji la Yola huko Adamawa, kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Nigeria ilitangazwa kuwa haina polio na WHO mwaka 2020 baada ya miaka mingi ya kampeni ya chanjo. Picha: Reuters

Na Charles Mgbolu

Wimbo huo, ulioandikwa katika lahaja asilia ya Fulfulde, unazungumzia kazi yao na lengo la kuhakikisha huduma za afya zinaenea hadi kwa jamii lengwa.

Ni wimbo unao kusudiwa kuongeza ujasiri kwa wafanyakazi hawa wanapo jitokeza kwa ajili ya harakati za chanjo ya umma ambayo itawapeleka baadhi yao katika maeneo ya ndani ya eneo hilo. Saa za barabarani haziwasumbui kama vile mhofu ya kitu kiovu kinacho nyemelea gizani wanaposafiri.

“Nasafiri hadi Mayo na Gombi, ambapo ni takriban saa mbili kutoka yalipo makazi. Kabla sijaenda, naomba Mungu ayalinde maisha yangu," afisa wa chanjo Dorothy Ezekiel, 26, anaiambia TRT Afrika.

"Ninajua ninahatarisha sana maisha yangu, kwa sababu kusafiri kwa barabara kwenda maeneo ya mbali kunaweza kukuongoza moja kwa moja kwenye mikono ya watekaji nyara, majambazi au hata magaidi.”

Wahudumu wa afya katika jimbo la Adamawa kwa kawaida hufanya safari ngumu kwenda maeneo ya mashambani kuwachanja watoto. Picha: Dorothy Ezikiel

Sekta ya Fidia

Matukio ya utekaji nyara kwa ajili ya kupata fidia yameongezeka sana nchini Nigeria, hasa kaskazini mwa nchi hiyo. Kulingana na data kutoka kwa Baraza la Mahusiano ya Kigeni, zaidi ya watu 4,000 walichukuliwa mateka nchini Nigeria mnamo 2022.

Zaidi ya watu 4,500 waliuawa. Mnamo Februari 3 pekee mwaka huu, wanawake 15 walitekwa nyara huko Kankara, jimbo la Katsina. Wengine saba waliuawa katika jimbo la Taraba kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Mnamo mwaka 2018, wafanyakazi watatu wa misaada walikuwa wamechukuliwa mateka na Boko Haram katika jimbo la Borno. Mwanajeshi mmoja alikuwa akiwasindikiza wafanyakazi wa kutoa misaada kutoka Maiduguri hadi Monguno walipovamiwa.

Wafanyakazi wa misaada hupeleka chakula na dawa kwa watu wengi waliokimbia makazi yao kutokana na migogoro.

Mnamo Juni 2022, Mratibu Mkazi na Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa aliambia vyombo vya habari vya ndani kuwa mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya wafanyakazi wa misaada, hasa karibu na Adamawa na jumuiya zinazo izunguka, yalikuwa yakikwamisha juhudi za kibinadamu katika eneo hilo.

Kulingana na ripoti ya Shirika la Kitaifa la Usimamizi wa Dharura la Nigeria, zaidi ya watu 230,000 walikuwa wakiishi katika kambi za IDP kwenye jimbo la Adamawa kufikia Julai mwaka jana wakati zaidi ya 780,000 walikuwa wamepewa makazi mapya hadi Machi.

Wengi wao waliokuwa katika kambi hizo walikuwa wamefurushwa kutoka katika jamii zao kutokana na ukatili wa majambazi wenye silaha, magaidi au watekaji nyara.

Wakihatarisha usalama wao binafsi, wafanyikazi wa afya katika mikoa hii wanaendelea kutoa msaada kwa watu hawa, wakisafiri kwenda maeneo yaliyo jitengwa, mara nyingi hayafikiki kirahisi. Wanafika huko kutoa chanjo na kusambaza dawa zinazo hitajika.

John Manabeta, mkurugenzi mtendaji wa kikundi cha utetezi wa jinsia kwa wanawake, anashangazwa na ujasiri waKatika maeneo mengi ya kaskazini mwa Nigeria, anti-vaxxers huweka upinzani mkali, na wakati mwingine vurugu, kwa wafanyakazi wa afya wanaojaribu kuwachanja watoto wao. wafanyakazi wa afya kutekeleza majukumu yao katika hali ya hatari.

Sadiq Musa, ambaye amekuwa akifanya kazi kama mfanyakazi wa afya anayetembea kwa muda wa miaka 29, anajua nini kinahitajika ili kukabiliana na hali hiyo.

Wengi wa watu waliokimbia makazi yao kutokana na usalama wa usalama kashazini Nigeria ni wanawake na watoto. Picha: kumbukumbu au AFP

"Wanasafiri katika vijiji hivi peke yao. Hawaendi na watu wa usalama au wasindikizaji...hakuna kitu. Wanaomba tu kurudi salama," anasema.

Kundi la Watu

Katika maeneo mengi ya kaskazini mwa Nigeria, anti-vaxxers huweka upinzani mkali, na wakati mwingine vurugu, kwa wafanyikazi wa afya wanaojaribu kuwachanja watoto wao.

Sadiq Musa, ambaye amekuwa akifanya kazi kama mfanyakazi wa afya muda wa miaka 29, anajua nini kinahitajika ili kukabiliana na hali hiyo.

"Mimi hukutana nao kila siku, na wananituhumu kwa kuwadunga watoto wao dawa za kuzuia mimba ili washindwe kuzaa watoto wengi," Afisa wa chanjo Dorothy anakumbuka wakati wa kutisha sana alipolazimika kukimbia jamii na mwenzake wa kike.

"Ghafla walianza kuzungumza katika lahaja mimi au mfanyakazi mwenzangu sikuielewa," anasimulia. "Walikuwa wanaume wanane, na ilionekana kuwa walikuwa wakijaribu kutuzunguka polepole.

Nilimwambia mwenzangu, 'Sisi inabidi kuondoka mahali hapa mara moja." Dorothy na mwenzake wakageuka na kuondoka haraka haraka wakakuta kundi la wanaume likiwafuatilia kwa mwendo uleule. "Moyo wangu ulikuwa ukipiga kwa kasi sana.

Walisimama baada ya muda lakini waliendelea kututazama huku tukienda mbali na eneo hilo," anasema.

Laurete Anaza, ambaye anafanya kazi na NGO inayotoa mafunzo kwa wahudumu wa afya wa kujitolea, aliiambia TRT Afrika kuwa matukio kama hayo, ingawa ni ya mbali sana, yanaweza kuharibu afya ya akili kwa mfanyakazi wa afya aliyeathirika.

"Ndiyo, tunawaambia wakimbie kuokoa maisha yao inapotokea hatari, hasa wakati kuna hatari ya madhara kwa mtu au mfanyakazi mwenzao. Tumesha pata kesi za kushambuliwa kwa wahudumu wa afya." John Manabeta, afisa mwingine, anathibitisha hili.

"Tunawaambia wahudumu wetu wa afya waweke alama kwenye nyumba walizokabiliwa na matatizo, na wakati mwingine tunarudi na maafisa wa polisi ikiwa kumekuwa na vurugu kubwa dhidi ya wafanyakazi."

Dorothy anasema yeye na wenzake walikuwa wamekumbana na hali 'ya kutisha' wakati wa kazi yao. Picha: Dorothy Ezekiel

Matukio ya mara kwa mara kama haya, ingawa hayapungui, hayajamkatisha tamaa Dorothy kuendelea na kazi ya kutoa huduma katika maeneo yenye uhitaji.

“Sijaweza kurejea katika jamii hiyo iliyokuwa na chuki dhidi yangu na mwenzangu."

Kwa wale wengine ambao nimesafiri kwenda kwao, nilikwenda nikiwa nimejitayarisha, nikiwa nimevaa viatu vya kukimbia na kaptula chini ya nguo zangu, na kubaki macho." Kazi Muhimu

Kulingana na WHO, chanjo kwa sasa inazuia vifo milioni 5 kila mwaka kutokana na magonjwa kama diphtheria, tetanasi, pertussis, mafua na surua.

Chanjo pia hupunguza hatari ya kupata ugonjwa kwa kufanya kazi ya kujenga ulinzi asili wa mwili. Kwa hivyo, kuwachanja watoto ni muhimu licha ya hatari za kiusalama zinazo wakabili wale wanaohusika katika kampeni.

Mnamo Machi mwaka jana, serikali ya jimbo la Adamawa ilitangaza kuwa imefanikisha kutoa chanjo kwa 100% dhidi ya magonjwa kama polio, kando na kutolewa kwa chanjo ya Uviko-19.

Wafanyakazi wa afya kaskazini mashariki mwa Nigeria wanapaswa pia kukabiliana na matatizo ya kibinadamu kutokana na migogoro. Picha: Reuters

Ni ushahidi wa ujasiri na kujitolea kwa wale walio husika katika zoezi hilo, jambo ambalo mfanyakazi wa afya Sadiq analijumuisha kwenye maombi yake.

"Hii ndiyo inanifanya nijivunie aina ya kazi ninayofanya," anasema. Kazi bado haijaisha. "Bado kuna jamii kwenye ukingo ambazo bado hazijafikiwa. Inaweza isiwe leo au kesho, lakini hakika tutapeleka ujumbe wetu wa afya kwao. Siku moja kwa uhakika," anasema Dorothy.

TRT Afrika